Empoli wapania kupata alama sita za msimu dhidi ya Juventus


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 27

Empoli FC v Juventus FC 

Stadio Carlo Castellani
Empoli, Italy 
Saturday, 26 February 2022
Kick-off is at 19h00  
 
Empoli FC watakuwa mwenyeji wa Juventus FC katika mechi ya ligi ugani Stadio Carlo Castellani tarehe 26 Februari.
 
Empoli walipoteza 2-0 mchezo uliochezwa Februari 19 ugenini dhidi ya UC Sampdoria
 
Empoli hawajashinda mechi yoyote katika mechi tisa za ligi zilizopita huku wakiandikisha sare tano na kushundwa mara nne.

Andrea La Mantia
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vile vile, Empoli hawajashinda mechi yoyote ya ligi nyumbani katika mechi nne zilizopita, wakiwa wameandikisha sare moja na kushindwa mechi tatu mfululizo.
 
Kwengineko, Juventus wakiwa nyumbani walitoa sare ya 1-1 dhidi ya Torino katika mechi iliyopita ya ligi ya tarehe 18 Februari.
 
Juventus hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika michezo 12 iliyopita huku wakiandikisha sare nne na kushinda mechi nane.
 
Vile vile, wameshinda mechi nne na kutoa sare tatu katika mechi saba za mwisho wakiwa ugenini.

Massimiliano Allegri
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Ukweli ni kwamba hatukucheza vizuri jioni ya leo pengine kwa sababu tulikuwa na ratiba ya mechi ngumu siku zilizopita. Alama moja itatutosha kwa leo,” alisema meneja wa Juventus Massimiliano Allegri baada ya sare hiyo.
 
"Kwa ujumla, mchezo haukuwa mbaya sana na matokeo hayo yanatusaidia kuendeleza msururu wa matokeo mazuri. Unahitaji umakini mkubwa katika michezo kama hii lakini leo tumefanya makossa madogo madogo. Hata hivyo, ni jambo la kawaida unapokuwa unajifundisha kama tunavyofanya sasa. Dusan Vlahovic hakuwa na mchezo mzuri lakini inaeleweka hasa baada ya kucheza mechi kila baada ya siku tatu. Paolp Dybala alipata jeraha kidogo na tutachunguza ukubwa wa hali hiyo siku zijazo.”
  
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Empoli na Juventus ilichezwa Oktoba 28 2021.
 
Empoli waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Juventus katika hali ya kushangaza. Mechi hiyo ilichezewa Allianz Stadium ambao pia unaitwa Juventus stadium.
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho za ligi

 
Mechi - 5
Empoli - 1
Juventus - 4
Sare - 0

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.


Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 

Published: 02/23/2022