Clippers na Rockets kuchuana katika mechi ya NBA


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

Los Angeles Clippers v Houston Rockets

2021-22 NBA Regular Season

Friday 18 February 2022
Crypto.com Arena, Los Angeles, California
Tip-off at 06:30  
 
The Los Angeles Clippers watamenyana vikali na Houston Rockets katika mechi ya NBA kwenye ukumbi wa Crypto.com Arena, Los Angeles jimbo la California nchini Marekani Ijumaa ya tarehe 18 Februari 2022. Mchezo unatazamiwa kuanza saa kumi na moja na nusu majira ya Afrika ya kati.

The Clippers wapo katika hatari ya kushuka mbali na nafasi za timu zitakazoshiriki mechi za mchujo Eastern Conference japokuwa wameongeza wachezaji Rodney Hood na Semi Ojeleyo kutoka Sacramento na kumtoa Serge Ibaka kwa Milwaukee. Vile vile, wamemuongeza Norman Powell atakayeungana tena na Kawhi Leonard waliocheza pamoja Toronto.

Tyler Herro
Hakimiliki ya picha: Getty Images


“Hatuwezi kuwashinikiza sana wageni kwa sababu hawajawa nasi kwa muda mrefu. Hata hivyo tutafanya vyovyote kupata ushindi,” Tyronn Lue alisema akiwazungumzia wachezaji wapya. Nilipendezwa na nilichoshuhudia kutoka kwao. Kwa ujumla, uwezo wao ni mkubwa.”

Kwa upande wa The Rockets, kwa sasa wapo katika nafasi ya chini ya Western Conference. Katika hatua hii ya msimu wanacheza kuhitimisha ratiba tu. Timu yao bado ni changa na wana muda wa kupata uzoevu siku zijazo

Paul George
Hakimiliki ya picha: Getty Images


“Mechi zetu zimukuwa nzuri mwanzoni na tumekuwa tukionyesha hari,” mkufunzi Stephen Silas alisema baada ya kupoteza mechi dhidi ya Toronto Rapters wiki iliyopita. “Haya yote yamekuwa wazi katika hawamu tofauti tofauti za mechi.”

“Tulikosa kutumia nafsi za wazi kabisa. Bahati haikuwa upande wetu hata kidogo,” aliongeza Kevin Porter.

Historia baina ya timu hizi mbili inaonyesha kuwa the Clippers na the Rockets wamekutana mara 206 kuanzia mwaka 1970-71; Houston wakishinda mara 124 dhidi ya 82 kwa faida ya Los Angeles. Mara ya mwisho timu hizi zilikutana mwezi Mei 2021 ambapo Rockets walishinda 122-115 wakiwa nyumbani. Kelly Olynyk na Jae’Sean Tate walichangia alama 20 kila mmoja.
 

Takwimu baina ya Los Angeles Clippers na Houston Rockets, NBA.  

Mechi: 206
Clippers: 82
Rockets: 124
 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 02/16/2022