Clippers kukutana na Lakers katika debi ya LA


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

Los Angeles Clippers v Los Angeles Lakers

2021-22 NBA Regular Season

Friday 4 February 2022
Crypto.com Arena, Los Angeles, California
Tip-off at 06:00  
 
The Los Angeles Clippers na Los Angeles Lakers watakutana katika debi ya LA mchezo wa kikapu, ugani Crypto.com Arena in L.A. California asubui ya Ijumaa Februari 4 2022. Mchezo utaanza saa kumi na moja asubui majira ya Afrika ya kati. 
 
The Clippers wanakaribia kufikia alama 500 katika msimu huu wa 2021/22 huku wakiwa na nafasi nzuri ya kufuzu mechi za mchujo. Misimu ya maajuzi, wamekuwa wakitoka nyuma na kushinda mechi zao hivyo basi kuwa timu hatari kwa wapinzani wowote. 

Lebron James
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Tumekuwa na mchanganyiko maalum wa wachezaji unaojumuisha wazoevu ambao wamekuwa katika mchezo huu kwa muda sasa na chipukizi wanaoibuka na kuonyesha uwezo wao kikamilifu,” alisema Eric Bledsoe. “Mchanganyiko huo unaleta timu kamilifu.”
 
"Maagizo yalikuwa, tuendelee kupambana. Huu ni utaratibu ambao tumeuanzisha hapa,” alisema Tyronn Lue. “Haijalishi nani amechaguliwa kucheza, hakuna visingizio vya aina yoyote bali tunapambana.” 
 
Uchezaji wa Lakers hauna utofauti mkubwa na Clippers japokuwa hauna viashiria kwamba wana hari ya kunyakuwa kombe la NBA tena. Wamekuwa wakimtegemea mchezaji LeBron James ambaye kwa sasa anasumbuliwa na jeraha la goti ambalo linaweza kumkalisha nje ya mchezo huu. 

Paul George
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
 “James ni kiungo muhimu katika mambo tunayofanya,” alisema mchezaji mwenzake Anthony Davis. “Inahuzunisha kumkosa lakini pia ni nafasi ya kujipima uwezo wetu asipokuwa uwanjani. Kwa hakika ni nafasi tutakayoichukuwa kwa mikono miwili.”
 
Historia inaonyesha kuwa Clippers na Lakers wamekutana mara 228 katika mechi mechi za NBA tangu 1970/1971. Clippers wameshinda mara 78 huku Lakers wakishinda mara 150. Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa Disemba 2021 ambapo Clippers wakiwa ugenini walishinda 119-115, alama 21 zikichangiwa na Marcus Morris. 
 

Takwimu baina ya Los Angeles Clippers na Los Angeles Lakers, NBA

Mechi: 228
Clippers: 78
Lakers: 150
 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 02/03/2022