Citizens kupiga hatua zaidi kuelekea ubingwa


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 26

Manchester City v Tottenham Hotspur

Etihad Stadium
Manchester, England
Saturday, 19 February 2022
Kick-off is at 20h30 
 
Manchester City wataialika Tottenham ugani Etihad Stadium katika mechi ya ligi Februari 19 huku wakipania kutetea ubingwa wa ligi.
 
Huku zikiwa zimesalia mechi 13 msimu kukamilika, City wanaongoza ligi, wakiacha nafasi ya pili kwa alama 9.
 
Vijana wa Guardiola waliichapa Norwich 4-0 katika mechi iliyopita, Februari 12 na kuendeleza msururu wa mechi bila kushindwa kuwa 15 huku 14 zikiishia kwa ushindi.

Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kevin De Bruyne, Joao Cancelo, Rodri na Aymeric Laporte hawakushiriki mechi hiyo dhidi ya Norwich huku Guardiola akisisitiza kuwa hakuna aliyetengewa nafasi katika kikosi cha kwanza na kwamba maamuzi yanategemea hali ya wakati huo.
 
"Kila mchezaji anastahili kucheza lakini maamuzi ni yang una hilo wanalifahamu,” alisema Guardiola.
 
"Hata unapocheza vizuri, kuna uwezekano husicheze mechi inayofuata kwa sababu kikosi ni kikubwa. Ni jukumu langu kuchagua kikosi kitakachotuwezesha kushinda mechi.
 
"Maamuzi yote yanafanywa kwa maslahi mapana ya timu. Klabu hii ni kubwa kuliko mtu yeyote. Lengo letu ni kushinda mechi kwa ajili ya mashabiki wanaosafiri kutoka sehemu tofauti kutushuhudia na kuhakikisha wanashuhudia mchezo mzuri.
 
"Kikubwa zaidi ni kila mchezaji kujituma kadri anavyoweza.”
 
Tottenham kwa upande wao, nafasi ya kuingia nne bora imezidi kuwa finyu kila uchao baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo. Aliposhika usukani, Conte alicheza mechi tisa bila kushindwa lakini baadaye akapoteza dhidi ya Chelsea 2-0, Southampton 3-2 na Wolves 2-0.

Antonio Conte
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Meneja wa Spurs amekiri kuwa itakuwa vigumu kuingia katika nne bora kwa hali waliyonayo sasa huku wakiwa katika nafasi ya nane na alama tano nyuma ya Westham united waliopo nafasi ya nne.
 
"Unapopoteza mechi mbili mfululizo ukiwa nyumbani na kupoteza mechi dhdi ya Chelsea, ni vigumu timu hiyo kuingia katika nafasi za kushiriki mechi ya mabingwa,” Conte aliiambia Sky Sports.
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Man City - 1
Tottenham - 3
Sarew - 1


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 02/16/2022