Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Spanish La Liga
Matchday 23
FC Barcelona v Atletico Madrid
Camp Nou
Barcelona, Spain
Sunday, 6 February 2022
Kick-off is at 18h15
FC Barcelona watakuwa mwenyeji wa Atletico Madrid ugani Camp Nou katika
mechi ya ligi mnamo Februari 6.
Katika mechi iliyochezwa Januari 23, Barcelona wakiwa ugenini waliishinda Deportivo Alaves 1-0.
Kufuatia ushindi huo, Barcelona hawajashindwa katika mechi tano zilizopita huku wakiambulia ushindi mara tatu na kupata sare katika mechi mbili.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Barcelona walirejelea mitindo ya ushindi katika mechi yao wakiwa nyumbani dhidi ya Elche baada ya Real Betis kuvunja msururu wao wa mechi mbili bila kushindwa.
"Ilitugharimu pakubwa lakini zilikuwa ni alama tatu muhimu ambazo kama timu tulizihitaji na tulifaa kuzipata,” alisema meneja wa Barcelona Xavi Harnandez walipoishinda Alaves.
"Huu ni mwanzo mpya na ushindi huu umeonyesha kuna matumaini ya kufanya vyema. Tunazidi kuimarika na tunaamini kazi tunayoendelea kuifanya.”
“Tupo katika mapambano. Kwa sasa tumebakisha alama moja hadi nafasi za kucheza ligi ya mabingwa. Tunaamini ipo siku ndoto zetu zitatimia.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwa upande mwingine, Atletico walitoka nyuma na kushinda Valencia 3-2 wakiwa nyumbani katika mechi ya ligi iliyopita ya Januari 22.
Atletico hawajashindwa katika mechi mechi tatu za ligi huku wakiwa wameshinda mechi mbili na kupata sare moja.
Hata hivyo, Atletico wamekuwa na matokeo duni wakiwa ugenini kwani wameshindwa mara tatu na kupata sare moja katika mechi nne wakiwa ugenini.
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya timu hizi ilikuwa Oktoba 2 2021.
Barcelona walipoteza mechi hiyo 2-0 ugani Wanda Metropolitano huku mabao hayo yakifungwa na Thomas Lemar na Luis Suarez.
Takwimu baina ya Barcelona na Atletico Madrid katika mechi tano zilizopita za ligi
Mechi - 5
Barcelona - 0
Atletico - 3
Sare - 2
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.