Atletico na Man United kukutana katika mechi rasmi


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 UEFA Champions League 

Round of 16 - First-Leg

Atletico Madrid v Manchester United 

Estadio Wanda Metropolitano
Madrid, Spain 
Wednesday, 23 February 2022
Kick-Off 23h00  
 
Atletico Madrid watakuwa mwenyeji wa Manchester United katika mechi ya mkondo wa kwanza wa mechi za UEFA raundi ya kumi na sita Februari 23. 
 
Mabingwa hao wa Uhispania walifuzu mechi za muondoano baada ya kunyakua nafasi ya pili ya kundi la B nyuma ya miamba wa soka Uingereza, Liverpool. 
 
Atletico waliicharaza FC Porto ya Ureno 3-1 katika mechi ya mwisho ya kundi B, ushindi ambao ulivunja msururu wa mechi tatu bila kushinda katika shindano hili. 

Yannick Carrasco
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Hata hivyo, Atletico hawajashinda mchezo wowote wa shindano hili wakiwa nyumbani huku wakiandikisha sare tatu na kushindwa mara tatu katika mechi sita. 
 
Manchester United waliipiku Villarreal ya Uhispania kuongoza kundi F hivyo basi kuingia hawamu ya muondoano ya UEFA.
 
Manchester United walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Young Boys ya Uswizi katika mechi yao ya mwisho ya kundi F na hawajapoteza mchezo wowote katika mechi tano zilizopita za mashindano haya. 
 
United wameandikisha ushindi mmoja na sare moja katika mechi mbili za shindano hili wakiwa ugenini. 

Luke Shaw
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Atletico Madrid wanajivunia wachezaji mahiri duniani kama vile Joao Felix, Luis Suarez na wengineo,” alisema mchezaji wa zamani wa United Owen Hargreaves baada ya droo kufanyika. 
 
"Jan Oblak ni mmoja kati ya walindalango wazuri kabisa duniani. Sio mchuano mkubwa sana kwa United lakini ni sawa na mchezo wa bahati na sibu. 
 
 “Utakuwa mchezo tutakaoshuhudia umahiri wa mbinu kati ya Rangnick na Simeone. Wachezaji wa Atletico wanapenda kucheza sana mchezo wa kushtukiza. 
 
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kabisa timu hizi kukutana katika mechi rasmi. 
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili

 
Mechi - 0
Atletico - 0
United - 0
Sare - 0


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 02/21/2022