Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi
Simba SC Salim Abdallah ‘Try Again’
ameweka wazi kuwa watahakikisha kuwa wanamuunga mkono Kocha mkuu wa kikosi chao Abdelakh Benchikha ili aendelee kuwapa raha ndani ya timu yao.
Kauli hiyo ni sawa na kumpa rungu kocha huyo ambaye alipanga mpango kazi kuwamaliza Wydad Casablanca kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Makundi wakishinda mabao 2-0.
Benchikha baada ya kutua ndani ya timu hiyo vitu vingi vimebadilika jambo ambalo limeonyesha kuwafurahisha mabosi wa timu hiyo ambao wamethibitisha ya kumsapoti ili aendelee kuwapa raha.
Try Again alisema kuwa “Tumeona ambacho kocha amekifanya ndani ya Simba SC na huyu ni kocha wa daraja kubwa na tayari kwa muda mupi tu ambao yupo ndani ya timu hii kuna vitu vimebadilika kuanzia uchezaji na hadi matokeo.
“Ukiangalia kwenye ligi watu wanahitaji matokeo lakini na timu iweze kufanya vyema kwa maana ya kuonyesha kiwango safi, lakini kwenye ligi ya mabingwa Afrika timu inatakiwa kupata matokeo haijalishi wamecheza katika kiwango gani.
“Sasa vyote hivyo vinapatikana kwa kocha huyo, kwetu sisi viongozi niweze kuweka wazi mbele ya hawa mashabiki wetu kuwa tutamuunga mkono kocha kwa kumpatia sapoti ya maana kwenye wachezaji ambao atawahitaji kwenye usajili wake ili kila kitu kiweze kwenda sawa, Simba SC tunahitaji kufurahi, “amesema kiongozi huyo.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.