Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji S Manara amefunguka kuhusu sakata lake la kufungiwa na Kamati ya Maadili ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kudaiwa kumtolea maneno machafu Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia.
Manara alifungiwa kujihusisha na soka kwa muda wa miaka miwili na faini ya Tsh milioni 10 tangu Julai 2022.
“Kwanza TFF wananidhulumu wao wanajua ,nchi inajua na kila mtu anajua lile tukio nilifanya mbele ya watu sikumtukana nimemwambia siondoki hili unanifanyia mara nyingi ,nilimjibu hivyo Karia ule ni mradi tu na mimi nakwambia nimefungiwa kwa sababu ya Simba “
“Hata ripoti yao inaeleza hakukuwa na matusi ,majibizano ndio umfungie mtu miaka miwili na milioni 20 ,mimi ni muungwana sijakukosea lakini nikaenda kumuomba radhi nyumbani kwake,” amesema Manara.
Aidha katika hatua nyingine,Haji Manara amesema kuwa baada kuteuliwa barbara Gonzalez kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo, yeye alimpigia simu Mohammed Dewji na kuomba aondoke.
Manara amesema alifanya hivyo kwa sababu alijua fika kuwa hatoweza kufanya kazi na dada huyo kutokana na tabia zake.
“Mo Dewji hana shida na mimi, mimi na yeye hatukuwahi kuwa na shida, kwanza Dewji anapenda watu wa aina yangu watu wanaoprotect timu lakini sasa wakawa wanamjaza kwamba Haji anakuwa maarufu kuliko wewe.
“Tukienda uwanjani mimi ninambwembwe na najua kujibrand siwezi kuingia uwanjani kabla uwanja haujajaa sasa ile wakawa wanamjaza kwamba wewe ndio unatoa hela lakini anasifiwa Haji, mimi nilimwambia hawa wanakujaza,” amesema Hajis Manara.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.