Serie A - AS Roma v SSC Napoli 


Hakimiliki ya picha: Getty Images


2023/24 Italian Serie A
Mchezo wa 17

AS Roma v SSC Napoli 

Stadio Olimpico
Rome, Italy 
Jumamosi Desemba 23 2023  
Muda: 9:45 pm
 
AS Roma itakabiliana na SSC Napoli katika mchezo wa kusisimua wa ligi kuu Italia ugani Stadio Olimpico Desemba 23.
 
Matokeo ya hivi karibuni
 
The Wolves, kama inavyojulikana Roma walipoteza 2-0 mikononi mwa Bologna FC ugenini mnamo Desemba 17 na kufikisha kikomo msururu wa mechi tano bila kushindwa kwenye ligi. 
 
Hata hivyo, Roma hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi Saba za ligi wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi wa mechi sita mfululizo na kutoa Sare moja ugani Stadio Olimpico.
 
Kwingineko, Napoli walishinda 2-1 kwenye mechi yao dhidi ya Cagliari FC wakiwa nyumbani Desemba 16. Walikuwa hawajapata ushindi katika mechi mbili za mwisho za ligi. 
 
Napoli maarufu kama the Little Donkeys walipoteza mechi yao ya mwisho ugenini dhidi ya Juventus FC, matokeo yaliyofikisha kikomo mechi nane mfululizo za ugenini bila kushindwa.
 
Vikosi
 
Roma watakosa huduma za Marash Kumbulla, Tammy Abraham, Chris Smalling, Paulo Dybala na Houssem Aouar ambao wanauguza majeraha.  
 
Kwa upande mwingine, Napoli watawakosa wachezaji Mathías Olivera, Piotr Zielinski na Eljif Elmas kwenye mechi hiyo kutokana na majeraha. 
 
Nukuu
 
“Ni timu inayotumia nguvu na kasi nyingi na hatukuweza kukabiliana na hali hiyo vilivyo. Ina wachezaji tofauti walio na sifa za kipekee,” alisema nyota wa Roma Leandro Paredes baada ya kupoteza mechi dhidi ya Bologna. 
 
“Unatakiwa kijutuma kwa nguvu nyingi muda wote jambo ambalo hatukufanya leo japo tulijitahidi. Tutajiandaa vilivyo kwa ajili ya mechi ijayo. Tunafahamu kuwa tuna mechi nne ngumu zijazo. 
 
“Ni jukumu letu kujiandaa vizuri kwa ajili ya kila mechi na kujiweka katika hali nzuri ili kukabiliana na wapinzani wetu bila kung’ang’ana sana.” 
 
Takwimu baina ya timu hizi
 
Napoli waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Roma timu hizi zilipokutana kwenye mechi ya ligi mnamo Januari 29 2023 ugani Stadio Diego Armando Maradona.
 
Napoli wameandikisha matokeo mazuri dhidi ya Roma katika michezo saba ya ligi iliyopita huku wakishinda mechi tano na kupata sare mbili. 
 

Ratiba ya mechi za Serie A mchezo wa 17.

  
Ijumaa, Desemba 22
 
7:30pm – Empoli FC v SS Lazio
7:30pm – US Sassuolo v Genoa CFC
9:45pm– AC Monza v ACF Fiorentina
9:45pm – US Salernitana v AC Milan
 
Jumamosi Desemba23
 
1:30pm – Frosinone Calcio v Juventus FC
4:00pm – Bologna FC v Atalanta BC
4:00pm – Torino FC v Udinese Calcio
7:00pm– Hellas Verona v Cagliari FC
7:00pm– Inter Milan v US Lecce
9:45pm – AS Roma v SSC Napoli


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Bashiri popote
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 12/20/2023