Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023/24 Spanish La Liga
Matchday 16
FC Barcelona v Girona FC
Estadi Olímpic Lluís Companys
Barcelona, Spain
Jumapili, Desemba 10 2023
Muda: 11:00pm
FC Barcelona watawaalika Girona katika
mechi ya ligi mnamo tarehe 10 Desemba ugani Estadi Olímpic Lluís Companys.
Matokeo ya hivi karibuni
Barca walipata ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Atletico Madrid Desemba 3 na kufikisha msururu wa mechi nne za ligi bila kupoteza hata moja.
Vile vile, Barcelona hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi mbili zilizopita wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi mara mbili mfululizo katika uwanja wao wa muda wa nyumbani Estadi Olímpic Lluís Companys.
Kwingineko, Girona walipata ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Valencia CF Desemba 2 na hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi nne zilizopita.
The White and Reds, kama inavyofahamika Girona hawajapoteza mechi hata moja ya ligi katika mechi saba za mwisho wakiwa ugenini huku wakishinda mechi sita na kupata sare moja.
Vikosi
Marc-Andre ter Stegen na Gavi wanazidi kuuguza majeraha kwa upande wa Barcelona ila hawana mchezaji anayetumikia marufuku.
Borja García, Toni Villa na Jastin García huenda wakakosa mechi hiyo kwa upande wa Girona kutokana na majeraha.
Nukuu
“Wachezaji walijituma sana chini ya shinikizo,” alisema kocha wa Barcelona Xavi Hernandez baada ya ushindi dhidi ya Atletico.
"Walizungusha mpira kwa weledi. Safu ya kati ikiwa na Ilkay Gündoğan, Pedri na Frenkie de Jong walielewana vizuri. Safu ya ulinzi ilikaba vizuri na Raphinha na Robert Lewandowski walitia bidii sana kwa ajili ya timu katika safu ya ushambuliaji.
“Tulikuwa na nafasi ya kufunga magoli zaidi mapema ila nimefurahishwa na nimeridhika na matokeo. Barcelona inafahamika kwa mtindo wa kucheza kama wa leo na inafaa kuwa hivyo kila wakati.”
Takwimu baina ya timu hizi.
Barcelona na Girona walitoa sare ya 0-0 kwenye mchezo wao mwisho wa ligi ugani Spotify Camp Nou Aprili 10 2023.
Barca hawajapoteza mchezo wa ligi dhidi ya Girona huku wakishinda mechi nne na kutoa sare mbili.
Ratiba ya mechi za La Liga mchezo wa 16:
Desemba 8, Ijumaa
11:00pm - Getafe CF v Valencia CF
Desemba 9, Jumamosi
4:00pm - Deportivo Alaves v Las Palmas
6:15pm - Real Betis v Real Madrid
8:30pm - Villarreal CF v Real Sociedad
11:00pm - Real Mallorca v Sevilla FC
Desemba 10, Jumapili
4:00pm - Atletico Madrid v UD Almeria
6:15pm - Granada CF v Athletic Bilbao
8:30pm - Cadiz CF v CA Osasuna
11:00pm - FC Barcelona v Girona FC
Desemba 11, Jumatatu
11:00pm - Rayo Vallecano v Celta Vigo
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.