IBRAHIM 'BACCA' APEWA FUPA LA AL AHLY...YANGA 'WAKISHITAKI' SIMBA CAF


KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, Yanga imesaini mkataba wa muda wa siku saba wenye thamani ya milioni 40 ikiwa ni milioni 20 kila siku.
 
Ni mkataba kati ya Yanga SC dhidi ya Zanzibar Investment Promotion Authority, (ZIPA) na Zanzibar Revenue Authority, (ZRA) ikiwa ni siku maalumu ambayo imepewa jina la BaccaDay.
 
Ni kuelekea mechi yao ya pili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly unaotarajiwa kuchezwa Desemba 2, 2023.
Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa watafanya kile ambacho kipo kwenye makubaliano.
 
“Yanga itafanya zaidi ya kile ambacho tumekubaliana katika mkataba huu.
Tumechagua kuja Zanzibar kwa lengo la kuzindua Bacca Day kwa sababu yeye ni mwenyeji wa hapa, lakini tumeenda mbali zaidi kwa kutumia tukio hili kuongeza mapato kwa Klabu yetu.
 
“Hivyo tumeingia mkataba na Zanzibar Investment Promotion Authority
(ZIPA) wenye thamani ya Milioni 20 pamoja na Zanzibar Revenue Authority
(ZRA) wenye thamani ya milion 20 kwa siku saba pekee.
 
  “Ni mara chache sana tunafanya mikutano na Wanahabari nje ya Dar es Salaam lakini kwa kipekee tumekuja Zanzibar kutokana na ubunifu wa kitengo cha Masoko na Habari kutoka kwenye klabu yetu,”
Ni kuelekea mechi yao ya pili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Al Ahly hapo Desemba 2, 2023.
 
Aidha katika hatua nyingine, Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema juzi taifa liliingia aibu baada ya Simba kupata sare na ASEC Mimosas na mashabiki kuingia wachache uwanjani.
 
Kamwe alisema, kwa kulitambua hilo, mashabiki wa Yanga watawaonesha ni namna gani uwanja unatakiwa ujae Jumamosi hii watakapokuwa wanacheza na Al Ahly katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.
 
"CAF wasifikiri labda kuna msiba kwa kuona wameingia mashabiki 66 kwenye ule mchezo, sisi tutaujaza uwanja kurejesha heshima maana sisi ndio wenye mpira huu nchini," alisema Kamwe.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Bashiri popote
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 12/01/2023