HIZI HAPA MBINU 'HARAMU' ZA BENCHIKHA ZILIZOIMALIZA WYADAD JANA


Benchikha alimtoa Chama nafasi yake ikachukuliwa na Israel Mwenda, akamtoa Kibu akaingia David Kameta, Abdallah Hamis aliingia kuchukua nafasi ya Mzamiru huku Baleke na kuingia Keneddy Juma.
 
Hii ni mara ya kwanza inaonekana kwenye timu ya Simba, Simba ikicheza na Fabrice Ngoma, Inonga, Che Malone, Israel Mwenda, Duchu, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein, Kennedy Juma, Mohammed Kazi na kipa Ayoub.
ikiwa ni mbinu pekee ya kulinda ushindi wake wa mabao mawili.
 
Baada ya kuingiza mabeki hao ambao wanne walikuwa wakicheza pembeni na wanne katikati, Wydad walifika langoni mwa Simba mara saba, lakini zote hakukuwa na madhara, huku mabeki wote wakifanya kazi kubwa ya kuokoa hatari, hata hivyo pamoja na kuwa na walinzi wengi Simba ndiyo walikosa nafasi ya wazi katika dakika ya 90 baada ya Inonga kushindwa kuuweka mpira kimiani ukatolewa na kuwa kona.
 
"Tunashukuru kwa kuwa tumepata ushindi napenda kuwapongeza wachezaji wangu wote kwa juhudi zao walizozionyesha, sasa tunajipanga kwa ajili ya michezo mingine," alisema Benchikha baada ya mechi.
 
Ayoub Lakred, Onana mastaa
_____________________________
 
Pamoja na Onana kufunga mabao hayo mawili, lakini ni dhahiri kuwa kazi kubwa sana kwenye mchezo huo ilifanywa na kipa Ayoub Lakred ambaye kipindi cha kwanza tu alifanikiwa kuokoa michomo mitano ambayo kama siyo umakini wake basi Simba ingeenda mapumziko kwa majonzi.
 
Hata hivyo kwa upande wa Onana, alikuwa shujaa kwenye mchezo huo akiwa amefunga mabao yake ya kwanza akiwa na Simba, lakini akiwa mchezaji wa kwanza kwa timu hiyo kufunga mabao mawili kwenye hatua ya makundi katika Uwanja wa Mkapa, mbali na kufunga lakini alifanikiwa kuonyesha kiwango cha juu, huku akipiga mashuti manne kwa dakika alizokaa uwanjani, kikiwa ni kiwango tofauti na huko nyuma.


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Bashiri popote
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 12/20/2023