Alamy hisa picha
2023/24 English Premier League
Matchday 14
Manchester City v Tottenham Hotspur
Etihad Stadium
Manchester, England
Jumapili, Desemba 3 2023
6:30pm Majira ya Afrika ya kati.
Manchester City wanapania kuibwaga Tottenham watakapokutana kwenye
mechi ya ligi ugani Etihad, Jumapili Desemba 3.
Spurs walianza msimu kwa matokeo mazuri huku wakicheza mechi za kwanza kumi bila kupoteza hata moja na kushika nafasi ya kwanza kwa wiki tatu mfululizo.
Hata hivyo, timu hiyo chini ya mkufunzi Ange Postecoglou ilipoteza mechi tatu mfululizo baadaye mikononi mwa Chelsea, Wolves na Aston Villa hivyo basi kushuka kwa kiwango kikubwa kwenye jedwali.
Baada ya kupoteza 2-1 nyumbani dhidi ya Villa mnamo Novemba 26, Tottenham walishuka hadi nafasi ya tano kwenye jedwali, alama nne chini ya viongozi wa ligi Arsenal
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Ushindi wa mechi 15 mfululizo wa City wakiwa nyumbani ulifikia kikomo baada ya kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Liverpool, ambao wamekuwa timu ya kwanza kupata alama ugani Etihad mwaka 2023.
Manchester City wanashika nafasi ya pili kwa sasa huku Arsenal wakichukua nafasi ya kwanza baada ya ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya Brentford.
Phil Foden alionyesha mchezo mzuri sana na kuwapa usumbufu mkubwa safu ya ulinzi ya Liverpool huku akipiga mashuti manne langoni mwa the Reds.
Spurs walitengeneza nafasi nyingi za kufunga dhidi ya Villa huku magoli matatu ya Son Heung-Min yalikataliwa kwa kuotea. Mshambuliaji huyo raia wa Korea Kusini amefunga magoli nane ya ligi msimu huu ila hajafanikiwa kufunga goli katika michezo mitatu iliyopita.
Guardiola alikiri kufurahia matokeo dhidi ya Liverpool baada ya mchezo wa kusisimua na kuwadhibiti wapinzani hao kwa nyakati ndefu za mechi hiyo.
"Hatuna furaha lakini ulikuwa mchezo wa kuvutia,” alisema raia huyo wa Uhispania. “Haijalishi timu ipi iliyokuwa na takwimu za kuvutia au nani alicheza vipi. Nitasherehekea kwa glasi ya mvinyo.
"Nimefurahishwa sana na juhudi zetu kwa sababu Liverpool ni timu nzuri sana. Tuliwadhibiti vizuri kwa sababu walipata nafasi mbili tu; shambulizi la kichwa kipindi cha kwanza na goli walilofunga.
"Ulikuwa ni mchezo mzuri kabisa na wa kusisimua baada ya miaka minane. Najivunia wachezaji wangu. Tunamiliki mpira muda wote. Tuomeonyesha mchezo mzuri kabisa baada ya miaka minane kwa maoni yangu.”
Postecoglou alisifia tena juhudi za timu yake na kusisitiza kuwa hakugadhabishwa baada ya timu hiyo kupoteza mchezo wa tatu mfululizo.
"Hayakuwa matokeo mazuri lakini nimefurahishwa na mchezo mzuri walioonyesha wachezaji wangu. Wamenifurahisha sana,” aliambia Sky Sports. “Nahisi tulicheza mchezo wa kusisimua na kuna uwezekano tungeshinda mchezo huo kirahisi kabisa.
"Walionyesha juhudi, nia na kujituma vilivyo. Sina gadhabu. Tulicheza mchezo mzuri na hilo ndilo nahitaji kama kocha.
"Sio kila wakati utafanikiwa ila kama mkufunzi unazingatia juhudi za wachezaji kufanikisha malengo tuliyoweka na leo wameonyesha hilo kwa asilimia mia moja.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Matches - 5
Man City - 2
Tottenham - 3
Draws - 0
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 14.
Jumamosi, Desemba 2
5:00pm: Arsenal v Wolverhampton Wanderers
5:00pm: Brentford v Luton Town
5:00pm: Burnley v Sheffield United
7:30pm: Nottingham Forest v Everton
10:00pm: Newcastle United v Manchester United
Jumapili, Desemba 3
4:00pm: Bournemouth v Aston Villa
4:00pm: Chelsea v Brighton & Hove Albion
4:00pm: Liverpool v Fulham
4:00pm: West Ham United v Crystal Palace
6:30pm: Manchester City v Tottenham Hotspur
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.