BENCHIKHA APANGA KUWAFANYIA 'MAJAMBOZI' MASTAA SIMBA


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo


KOCHA wa Simba, Abdelhak Benchikha amekiri kuna mambo mengi anatakiwa kuyafanyia kazi ili kikosi chake kiwe imara, baada ya kuiongoza kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Jwaneng Gallaxy katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika.
 
Benchikha amesema ameona timu yake ilivyocheza, lakini bado ana kazi kubwa ya kufanya maboresho ndani ya kikosi hicho kwa kuongeza wachezaji ambao watafanikiwa kwenye malengo yao.
 
Kauli ya Benchikha inamaana kubwa ya Simba kufanya maboresho makubwa kupindi cha usajili wa dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa mwenzi huu kwa klabu kuimarisha vikosi vyao na kujiweka imara katika michezo iliyopo mbele yao ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
 
Benchikha mapema juzi alianza kuinoa rasmi Simba tangu alipokabidhiwa mikoba ya Roberto Oliviera (Robertinho).
 
Katika mchezo huo, Simba walipata sare ya bila kufungana ikiwa ni ya pili kwenye michuano hiyo baada ya mechi ya kwanza kutoka sare ya 2-2 na Asec Mimosas ya Ivory.
 
Benchikha amesema kuna mambo mengi ya kufanyia kazi ili Simba irejee katika ubora wake.
 
Amesema kwa sasa anaangalia kila uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na kujiridhisha kabla ya kufanya usajili kipindi cha dirisha dogo ambalo anahitaji kuongeza watu.
 
“Nimeona mapungufu ambayo tunaenda kuyafanyia kazi kwa wachezaji waliopo sasa, lakini kuna mambo mengi ya kubadilisha na kuboresha kikosi changu kulingana na changamoto nilizoziona katika mchezo wa leo (juzi) ikiwemo kutumia nafasi zinazopatikana.
 
Tulikuwa na uwezo wa kufunga bao lakini hatukuwa makini ndio mpira na kwenda kusahihisha ili kujiweka imara kwa mechi zijazo ikiwemo dhidi ya Wydad Casablanca,” amesema Benchikha.
 
Ameongeza kuwa walistahili kupata alama tatu kwa sababu walicheza vizuri muda mwingi na kutengeneza nafasi lakini katika mita chache kutokana eneo la Jwaneng Galaxy hawakuwa bora.
 
“Sijafurahishwa na matokeo ya sare kwa kuwa anamini kwa kuwango tulichoonyesja tulistahili kushinda, tumecheza vizuri karibia kila idara, shida ilikuwa katika eneo la tatu la wapinzani tulipoteza umakini uliotufanya kukosa nafasi nyingi,” amesema Benchikha.
 
Kuhusu matumaini ya kwenda robo fainali, kocha huyo alisema kundi bado liko wazi timu yoyote ina nafasi ya kusonga mbele , Simba wanajipanga kwa ajili ya michezo yao ijayo.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Bashiri popote
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 12/11/2023