KOCHA mkuu wa
Simba, Abdelhak Benchikha ameanza kuonyesha makucha yake na kusema hatoangalia ukubwa wa jina la mchezaji au kipenzi cha nani zaidi ya kutaka kuona kiwango bora na kupambania klabu hiyo kufikia malengo.
Itafahamika kuwa Chama ndiye kipenzi cha mashabiki wengi wa Simba huku akiwa pia na ushawishi kwa wachezaji wenzake, hivyo mkwara wa Bencikha kwa namna moja au nyingine yeye pia anahusika.
Kocha huyo alisema malengo yao ni kufanya vizuri lazima mchezaji anatakiwa kupambana na sio kujiona mkubwa ndani ya timu kwa sababu malengo lake kubwa ni kuifanya timu hiyo kupata ushindi uwanjani na kutwaa mataji mbalimbali ya ligi ya ndani na kufikia malengo katika michuano ya kimataifa.
Alisema ili timu kupata mafanikio lazima kuwepo kwa mshikamano baina ya timu, viongozi na mashabiki kwa ujumla, mashabiki wanatakiwa kusapoti timu yao.
"Kuna vingi navijua nimekuja na mikakati yake na atapata nafasi ya kuona wachezaji wake na kuangalia yupi anamfaa au hamfai. suala la mashindano ninaimani nitafanikiwa kufanya vizuri kwa sababu mimi ni mpambanaji,"
alisema Benchikha.
Aliongeza kuwa anaimani atawafurahisha mashabiki kwa kutengeneza Simba mpya na imara kikubwa anahitaji sapoti na ushirikiano mkubwa kutoka kwao na kufanikisha kile ambacho wanakitarajia.
Kocha huyo alisema amekuja kwa malengo ya kufanikiwa kwa klabu ya Simba kama ilivyo kwa klabu alizotoka kubwa zaidi ni ushirikiano mkubwa hasa kwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Iman Kajula alisema wametamatisha shauku ya mashabiki kumpta mwalimu, walipokea wasifu nyingi kutoka kwa makocha mbalimbali lakini walikuwa na kipindi kigumu kupata kocha mzuri kama ilivyo kwa Benchikha.
"Benchikha atakuwa Simba kwa mkataba wa miaka miwili, atamalizia msimu huu na msimu ujao, mashabiki wanatakiwa kuwa watulivu kwa sababu kocha mpya, viongozi tumempa uhuru wa kufanya kazi na hatuna utaratibu wa kumpangia kocha kupanga kikosi nani acheze na asicheze," alisema Kajula.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.