KIFAA HIKI KIPYA KUTOKA MOROCCO NACHO KINATUA MSIMBAZI...


WAKATI Simba inashuka dimbani kesho dhidi ya Kagera Sugar, Uongozi wa timu hiyo umefunga kuhusu kuhusishwa na usajili wa nyota watatu, Lameck Lawi wa Coastal Union na Ladack Chasambi kutoka Mtibwa Sugar na Eric Mbangossoum kutoka Union Touarga Sportif ya Morocco .
 
Umesema ni mapema kuzungumzia usajili ya kwa sababu benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Abdallah Benchikha anafanya tathimini juu ya wapi kufanyia kazi na nani wataingia katika dirisha hilo.
 
Tayari Simba inakuhusisha kumalizana na nyota wawili, mmoja ni mzawa ambaye ni Chasambi na Eric wanaotajwa kuwa miongoni mwa nyota ambao watajiunga na kikosi cha wekundu hao katika usajili ya dirisha dogo lililofunguliwa leo.
 
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, amesema zoezi lote la usajili liko mikononi mwa kocha Benchikha ambaye amefanya tathimini ya kikosi chake na kuona wapi na nani anaweza kuongeza nguvu.
 
“Kwa sasa ni mapema sana kuzungumza lolote juu ya usajili na nani anaingia au kutoka, hilo ni jukumu la kocha ambaye amefanya tathimini ya timu yake na tunatarajia kupata mapendekezo juu ya nafasi na wachezaji wataongezwa nguvu.
 
Muda ukifika kila kitu kitawekwa wazi kwa sasa akili na nguvu zetu kuelekea mechi zilizopo mbele yetu, tunakibarua kigumu cha kutafuta pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar baada ya hapo kuna Wydad Casablanca kuwapeleka moto hapa nyumbani na kuacha alama ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” Amesema Ahmed.
 
Kuelekea mchezo wao dhidi Kagera Sugar unaotarajia kucheza leo saa 10:00 alasir, uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Kocha Benchikha amesema baada ya safari ndefu kutoka Morocco wamerejea na kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kuvuna alama tatu katika mchezo huo aa ligi kuu.
 
Amesema amepata fursa ya kuona taarifa za wapinzani wao na ameaandaa kukosi chake kwa ajili ya ushindani mkubwa kulingana na ubora wa mchezo huo.
 
“Tunahitaji ushundi tunawaheshimu wapinzani wetu , kwa upande wangu hii mechi ni muhimu sana baada ya hapa nitaifikiria Wydad Casablanca. Hakuna mechi rahisi na kila mchezo umekuwa na maandalizi yake.
 
Kuwepo kwa mfululizo wa mecho kla baada ya siku mbili au tatu hilo haitakuwa na athari kikubwa ni kuandaa timu kulingana na mpinzani unayekwenda kucheza naye,” amesema Benchikha.
 
Mwakilishi wa wachezaji kwa upande wa Simba, Ally Salim amesema wamejiandaa vizuri kwenda kuwakabili wapinzani wao Kagera Sugar kuhakikisha wanafanikiwa kuvuna alama tatu muhimu.

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Bashiri popote
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 12/20/2023