Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 FIFA World Cup
Last 16
France v Poland
Al Thumama Stadium
Doha, Qatar
Sunday, 4 December 2022
Kick-off is at 18h00
Katika azma ya kutetea taji la
kombe la dunia, Ufaransa itakabiliana na Poland Jumapili Desemba 4 kwenye mechi ya hatua ya 16.
Mabingwa hao wa mwaka 2018 walianza kampeni ya mwaka huu vizuri kwa kuishinda Australia 4-1 katika mechi ya ufunguzi ya kundi D kabla ya kuishinda Denmark 2-1.
Chini ya kocha Didier Deschamps, Ufaransa ilipoteza 1-0 dhidi ya Tunisia katika hali ya kutatanisha Jumatano Novemba 30 japokuwa walifanikiwa kuongoza kundi hilo.
Tunisia walipata bao dakika ya 58 kupitia mchezaji Wahbi Khazri na Les Bleus walidhani wamepata bao la kusawazisha katika dakika za nyongeza kupitia Antoine Griezmann.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Hata hivyo, bao hilo lilikataliwa baada ya kutazamwa tena kwa makini kupitia mtambo wa VAR.
Deschamps alitetea uamuzi wake kuwaacha nje wachezaji Griezmann, Kylian Mbappe, Ousmane Dembele na Hugo Lloris dhidi ya Eagles of Carthage akisema kuwa walihitaji mapumziko.
"Hatuwezi kupata kila kitu sahihi. Muhimu zaidi ilikuwa kufuzu hatua ya 16,” alisema. “Wachezaji wote 24 walishinda mechi za kwanza mbili na kupoteza mechi ya mwisho ila nawahitaji wachezaji wote 24 ndani ya siku nne.
"Baadhi wamepata muda wa kupumzika. Tumemaliza kucheza mechi mbili ngumu sana. Tutacheza mechi nne ndani ya siku 12 na tulihitaji kupumzika.
"Tunastahili kucheza vizuri kuliko tulivyocheza. Mpinzani wetu alifanikiwa kutubana na kupata bao. Sikumdharau mpinzani, sikuidharau mechi. Mawazo yangu yalikuwa kwenye mechi inayotungoja Jumapili.”
The Eagles ya Poland ilifuzu kuingia hatua ya 16 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986 licha ya kupoteza mchezo wa tatu 2-0 dhidi ya Argentina.
Poland walimaliza katika nafasi ya pili kundi C na alama nne baada ya kupata sare ya 0-0 mechi ya kwanza dhidi ya Mexico na kushinda mechi ya pili 2-0 dhidi ya Saudi Arabia. Mexico walimaliza mechi za makundi na alama nne vile vile lakini Poland waliwazidi kwa ubora wa magoli.
Vijana wa Czeslaw Michniewicz walinusurika kuaga shindano hili mapema baada ya Lionel Messi kukosa penalti dakika za mwanzo za mechi.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Michniewicz alikiri kuwa hali ilikuwa tete katika juhudi zao kufuzu hasa baada ya kadi ya njano ya Grzegorz Krychowiak dakika ya 78 ambayo ingekuwa kigezo cha kuamua atakayefuzu kati ya Poland na Argentina.
"Tulikuwa na makubaliono kuwa ni mimi tu na wasaidizi wangu tutafuatilia kinachoendelea kwenye mechi ya Mexico,” alisema.
"Nilipata mshtuko kidogo Grzegorz Krychowiak alipoonyeshwa kadi ya njano. Tulifahamu inaweza kutugharimu alama tatu ukizingatia sheria za idadi ya kadi za njano zinazotolewa.
"Tulitaka kupumzisha Piotr Zielinski lakini tukamtoa Krychowiak kwa kuwa kwa dakika tano hatukuweza kudhibiti mpira na ilikuwa vigumu kufanya mabadiliko. Vile vile, Grzegorz Krychowiak alikuwa katika hatari ya kupokea kadi nyekundu.
"Benchi langu la ufundi lilinijulisha kuwa kulikuwa na tofauti ya kadi mbili au tatu za njano kwa hivyo tulitakiwa kuwa makini sana. Tulikuwa katika wakati mgumu mechi ilipokuwa 2-0. Niliwaagiza kuepuka kadi zisizo na maana. Tulifanya juhudi kuepuka matukio ya utovu wa nidhamu au kubishana na mwamuzi.”
Takwimu baina ya timu hizi
Mechi - 16
Ufaransa - 8
Poland - 3
Sare - 5
Shinda na Kombe la Dunia
Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.