Shindano la gofu Hero World Challenge 2022 kung’oa


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 Hero World Challenge

US PGA Tour (Unofficial event)

Albany Golf Course
Albany, New Providence, The Bahamas
1-4 December 2022

Shindano la 2022 Hero World Challenge la gofu litafanyika Albany, New Providence, The Bahamas kati ya tarehe 1 na 4 Desemba.

Shindano hili lilianzishwa mwaka 2000 na Tiger Woods na hushirikisha idadi ndogo ya wachezaji wakubwa wa gofu, kwa sasa idadi hiyo ikiwa 20.

Shindano hili ni sehemu ya PGA Tour japokuwa haichangii alama za FedEx Cup au zawadi rasmi ya fedha kwa sababu sio shindano rasmi.

Justin Thomas
Hakimiliki ya picha: Getty Images


Viktor Hovland ndiye bingwa wa sasa baada ya kushinda shindano la mwaka jana la Hero World Challenge alipomshinda Scottie Scheffler kwenye mechi ya mchujo.

Shindano la Hero World Challenge 2022 litahusisha Hovland na washindi wengine sita ambao wameshinda mashindano 10 kwa pamoja.

Hovland, Scheffler, Jon Rahm, Xander Schauffele, Justin Thomas, Collin Morikawa, Matt Fitzpatrick, Sam Burns, Jordan Spieth na Tony Finau watashiriki.

Woods alitarajiwa kushiriki lakini akajiondoa siku chache kabla kutokana na jereha la mguu.

Mshindi wa shindano hilo atakabidhiwa dola milioni 3.5 za kimarekani.

Collin Morikawa
Hakimiliki ya picha: Getty Images


"Katika kujiandaa kwa ajili ya shindano la Hero World Challenge wiki hii, nilipata uvimbe kwenye mguu wangu wa kulia, plantar fasciitis hivyo basi ni vigumu kwangu kutembea,” alisema Woods Jumatatu.

"Baada ya kujadiliana na madaktari na walimu wangu, nimefikia maamuzi ya kujiondoa wiki hii na kujikita katika shughuli za uandaaji.

"Mpango wangu ni kushiriki mashindano ya The Match na PNC."

Woods ndiye mchezaji mwenye mafanikio makubwa katika historia ya shindano la Hero World Challenge akiwa na mataji matano tangu shindano lilipoanzishwa mwaka 2000.
 

Washindi watano wa mwisho wa shindano la Hero World Challenge


2016 - Hideki Matsuyama - Japan
2017- Rickie Fowler - Marekani
2018 - Jon Rahm - Uhispania
2019 - Henrik Stenson - Uswidi
2021 - Viktor Hovland - Norway
 

Shinda na Kombe la Dunia

Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 
 
 

Published: 12/01/2022