Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 Spanish La Liga
Matchday 15
Atletico Madrid v Elche CF
Estádio Cívitas Metropolitano
Madrid, Spain
Thursday, 29 December 2022
Kick-off is at 23h30
Atletico Madrid watakabiliana na Elche CF katika mechi ya ligi kuu Uhispania
ugani Estádio Cívitas Metropolitano mnamo Desemba 29.
The Mattress Makers, kama wanavyofahamika Atletico Madrid walipoteza 1-0 dhidi ya
Real Mallorca ugenini katika mechi yao ya mwisho ya ligi Novemba 9.
Atletico Madrid hawajashinda mechi yoyote ya ligi katika mechi tatu zilizopita huku
wakipoteza mechi mbili na kupata sare moja.
Katika mechi tatu za mwisho za ligi wakiwa nyumbani, Atletico Madrid wamepata sare
mbili mfululizo na kushinda mechi moja.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwengineko, Elche walipoteza 2-1 nyumbani dhidi ya Girona FC kwenye mechi yao ya
mwisho ya ligi Novemba 8.
kufuatia matokeo hayo, Elche hawajapata ushindi katika mechi 14 za ligi huku
wakiandikisha sare nne na kupoteza mechi kumi.
Vile vile, Elche hawajapata ushindi katika mechi tisa za mwisho za ligi wakiwa ugenini
baada ya kupoteza mechi saba na kupata sare mbili, jambo linalowatishia kushushwa
daraja.
“Naamini hatutashushwa daraja kwa sababu nimekumbana na hali kama hii awali,”
kocha mpya wa Elche Pablo Machin alisema Novemba 30 baada ya kukabidhiwa
mikoba ya kunoa timu hiyo.
“Sikufahamika sana nikiwa Soria lakini nilipata fursa ya kufundisha Girona. Nilipambana
sana kusalia katika ligi. Siku kumi na tatu ligi kukamilika nilikuwa alama nane chini ya
mstari wa kushushwa daraja lakini tulifanikiwa kuokoa timu na janga hilo.
“Je nina mbinu za kuzuia janga hilo? Nina busara lakini mbinu hutofautiana kwa sababu
timu ni tofauti. Cha msingi ni kufanya kazi kwa juhudi na kujiamini kwa sababu kikosi
cha Elche ni kizuri tofauti na motokeo yao kwenye jedwali.”
Mara ya mwisho Atletico na Elche kukutana katika mechi ya ligi ilikuwa Mei 11 2022.
Atletico waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Elche katika mechi iliyochezewa ugani Estadio Manuel Martínez Valero, ambao ni uwanja wa pili kwa ukubwa Valencia.
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Atletico - 5
Elche - 0
Sare - 0
Ratiba ya mechi za La Liga mchezo wa 15.
Desemba 29 Alhamisi
7:00pm - Girona FC vs Rayo Vallecano
9:15pm - Real Betis vs Athletic Bilbao
11:30pm - Atletico Madrid vs Elche CF
Desemba 30 Ijumaa
7:00pm- Getafe CF vs Real Mallorca
9:15pm- Celta Vigo vs Sevilla FC
9:15pm- Cadiz CF vs UD Almeria
11:30pm - Real Valladolid vs Real Madrid
Desemba 31 Jumamosi
4:00pm - FC Barcelona vs RCD Espanyol
6:15pm - Real Sociedad vs CA Osasuna
6:15pm - Villarreal CF vs Valencia CF
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.