Morocco wapania rekodi zaidi mechi ya nusu fainali dhidi ya Ufaransa


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIFA World Cup

Semi-finals

France v Morocco

Al Bayt Stadium
Al Khor, Qatar
Wednesday, 14 December 2022
Kick-off is at 21h00  

Morocco inatarajia kuandikisha rekodi mpya ya kombe la dunia watakapokutana na mabingwa watetezi Ufaransa Desemba 14 Jumatano kwenye mechi ya nusu fainali.

The Atlas Lions ya Morocco iliandikisha historia ya kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufika hatua ya nusu fainali katika historia ya kombe la dunia walipoifunga Ureno 1-0 kwenye mechi robo fainali wikendi iliyopita.

Chini ya mkufunzi Walid Regragui, Morocco ilipenya kutoka mechi za makundi bila kupoteza mechi yoyote na wameruhusu goli moja tu hadi kufikia sasa katika mechi tano za shindano hilo linaloandaliwa Qatar.  Yassine Bounou amekuwa mlinda mlango wa kwanza kutoka Afrika kutoruhusu goli katika mechi tatu za shindano moja.

Yassine Bounou of Morocco
Hakimiliki ya picha: Getty Images


Bounou alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi kwenye mechi hiyo dhidi ya Selecao ya Ureno baada ya kuokoa mashuti makali ya mchezaji Joao Felix na Cristiano Ronaldo ambayo pengine yangepeleka kwenye muda wa ziada kufuatia goli la Youssef En-Nesyri dakika ya 42.

Regragui amelinganisha mafanikio ya Morocco katika shindano la hili la Qatar na Rocky Balboa wa sinema ya Rocky na kusema kuwa timu yake kuonekana wanyonge imechangia mashabiki wengi kuwa upande wao.

"Tunachukua nafasi ya Rocky Balboa katika shindano la mwaka huu,” alisema. “Timu yetu inapendwa zaidi katika shindano hili kwa sababu tunaonyesha ulimwengu mzima kuwa unaweza kufanikiwa hata unapokuwa huna talanta kubwa na fedha.

"Sio miujiza. Wengi watesema ni miujiza hasa katika bara Ulaya lakini tumeishinda Ubelgiji, Uhispania na Ureno bila kuruhusu goli. Tumeletea sifa watu wetu, bara letu na watu wengi sehemu tofauti. Unapotazama sinema ya Rocky utamuunga mkono Rocky Balboa."

Les Bleus ya Ufaransa waliendeleza azma yao ya kutetea taji hili kwa ushindi wa 2-1 katika mechi ya robo fainali dhidi ya Uingereza. Olivier Giroud aliwapa ushindi kupitia bao la dakika ya 78 baada ya Harry Kane kusawazisha goli la mapema la mchezaji Aurelien Tchouameni.

Vijana wa Didier Deschamps walibahatika Harry Kane aliposhindwa kufunga penalti zikiwa zimesalia dakika sita mchezo kukamilika japokuwa Ufaransa ilipambana vilivyo na sasa watakutana na Morocco.

Olivier Giroud
Hakimiliki ya picha: Getty Images

Suggested photo: Olivier Giroud of France

"Ni fahari kwa wachezaji hawa kufika hatua ya nusu fainali tena,” alisema Deschamps. “Tulibahatika kwa kiasi fulani. Tulisababisha penalti mbili lakini tulilinda ushindi wetu kwa nguvu nyingi.”

Deschamps amewaonya wachezaji wake kutowapuuza Morocco ambao tayari wamepata ushindi dhidi ya timu kubwa kama Ubelgiji, Uhispania na Ureno katika shindano hili.

"Sio wengi waliotarajia Morocco kuwa hapa leo lakini wamedhihirisha vinginevyo na sio ajabu. Wameruhusu goli moja tu katika mechi tano. Wana kila haki ya kuwa hapa.” Aliambia Telefoot.

Takwimu baina ya timu hizi

Mechi - 4
Ufaransa - 2
Morocco - 1
Sare - 1


Shinda na Kombe la Dunia

Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 


 

Published: 12/13/2022