Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 FIFA World Cup
Quarter-finals
Morocco v Portugal
Al Thumama Stadium
Doha, Qatar
Saturday, 10 December 2022
Kick-off is at 18h00
Morocco inalenga kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufika hatua ya nusu fainali ya
kombe la dunia watakapo kabiliana na Ureno ugani Al Thumama, Doha Desemba 10 Jumamosi.
The Atlas Lions ya Morocco iliwashangaza wengi walipoibandua Uhispania Jumanne iliyopita kupitia matuta ya penalti mechi yao ya hatua ya 16 bora ilipoishia sare ya 0-0 muda wa ziada.
Morocco chini ya Walid Regragui hawajapoteza mechi katika shindano hili. Wameruhusu goli moja tu hadi kufikia sasa na waliibuka wa kwanza kundi F baada ya kuishinda Ubelgiji ambao wanashikilia nafasi ya pili duniani katika jedwali la FIFA.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Regragui na wachezaji wake wanazidi kutimiza ndoto baada ya kuingia hatua ya robo fainali, ikiwa ni taifa la kwanza la kiarabu kuwa na mafanikio haya katika historia ya shindano hili.
"Niliwaambia wachezaji wangu kuwa ni mafanikio ya kufurahia,” alisema. “Ni mafanikio ambayo pengine hatutaweza kufanikisha tena.
"Binafsi sikufanikiwa kucheza kombe la dunia lakini sasa Mungu amenipa fursa kuandikisha historia kama mkufunzi. Nina furaha kubwa sana.
"Nahisi waafrika tunayo nafasi. Tuna uwezo wa kushinda kombe hili. Tunataka kuonyesha kizazi kijacho kuwa uwezo wanao.”
The Selecao ya Ureno watajaribu sana kuepuka yaliyowakumba majirani wao wa Iberia ambao licha ya kumiliki mpira kwa asilimia 77 walikosa mbinu za kupenya safu ya ulinzi ya Morocco.
Ureno chini ya Fernando Santos ilifanya kazi nyepesi dhidi ya Uswizi kwenye mechi ya hatua ya 16 bora hasa baada ya kupoteza 2-1 mikononi mwa Korea Kusini katika mechi ya mwisho ya makundi.
Cristiano Ronaldo hakuanza mechi hiyo huku nafasi yake ikichukuliwa na Goncalo Ramos aliyefunga magoli matatu na kusaidia kupatikana ushindi wa 6-1. Magoli mengine yalifungwa na Pepe, Raphael Guerreiro na Rafael Leao.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Santos alisisitiza kuwa nahodha wake ana mchango mkubwa katika timu ya taifa licha ya kuanza mechi dhidi ya Uswizi kama mchezaji wa akiba.
"Tumeshatatua mambo yetu na Ronaldo. Nilisema hili kwenye mkutano uliopita na wanahabari kwamba tumeshamaliza haya,” alihakikisha.
"Tukiangalia historia na takwimu za mchezaji huyu, ni mmoja kati ya wachezaji bora ukizingatia magoli na kama nahodha. Muhimu ni kuangalia maslahi mapana ya timu.
"Nimekuwa na uhusiano mzuri na wa karibu siku zote tangu akiwa na timu ya Sporting akiwa na miaka 19. Alianza kuchezea timu ya taifa na uhusiano uliendelea kukua zaidi.
"Hatuwezi kuwakilisha vibaya utu na uhusiano binafsi baina ya mkufunzi na mchezaji. Kwangu mimi atakuwa mchezaji muhimu sana kuwa naye kwenye timu.”
Takwimu baina ya timu hizi.
Mechi - 2
Morocco - 1
Ureno - 1
Sare - 0
Shinda na Kombe la Dunia
Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.