Macho yote kuangazia shindano la 2022 la Alfred Dunhill Championship


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 Alfred Dunhill Championship

Sunshine Tour 

European Tour
Leopard Creek Country Club
Malelane, Mpumalanga, South Africa
8-11 December 2022 
 
Shindano la gofu la mwaka 2022 la Alfred Dunhill Championship linatarajiwa kufanyika Malelane, Afrika Kusini kati ya tarehe 8 na 11 mwezi Desemba.
 
Shindano hili linasimamiwa na European Tour ikishirkiana na Sunshine Tour baada ya kuasisiwa mwaka 2000 mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
 
Shindano hili linadhaminiwa na kampuni ya Uingereza Alfred Dunhill Limited na linarejea baada ya kutofanyika mwaka 2021 kufuatia jangwa la COVID-19.

Charl Schwartzel
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Christiaan Bezuidenhout ndiye bingwa wa sasa baada ya kushinda shindano la mwaka 2020 la Alfred Dunhill Championship, ikiwa ni mara yake ya kwanza kulishinda.  
 
Bezuidenhout, Ernie Els, Charl Schwartzel, Pablo Larrazabal na Louis Oosthuizen watakuwa miongoni mwa washiriki wiki hii kati ya mabingwa wa zamani wa shindano hili pamoja na mabingwa wengine.
 
Branden Grace atashiriki vile vile na ni mchezaji pekee kuwahi kushinda shindano la Alfred Dunhill Championship pamoja na shindano-ndugu la Alfred Dunhill Links Championship nchini Scotland.
 
Mshindi wa shindano hili la 5 katika ratiba ya 2023 European Tour na shindano la 22 katika ratiba ya 2022-23 ya Sunshine Tour atatuzwa Euro milioni 1.5.

Pablo Larrazabal
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Tunafurahi kutangaza kurudi kwa shindano la Alfred Dunhill Championship," alisema Thomas Abt, kamishna wa Sunshine Tour.
 
"Hili ni mojawapo ya shindano muhimu kwetu kwani linawakilisha upekee wa mchezo wa gofu Afrika katika sehemu inayotambulika vizuri.
 
"Tunafurahi sana kwamba wachezaji wataweza kushiriki kwa mara nyingine shindano la gofu la Alfred Dunhill Championship, Leopard Creek, 
 
"Na mashabiki wa gofu watapata nafasi nyingine kufurahia mbuga na mazingira ya Afrika Kusini kupitia runinga za kimataifa.”
 
Schwartzel ni mchezaji menye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya shindano hili la Alfred Dunhill Championship akiwa na mataji manne.
 

Washindi watano wa mwisho wa shindano la Alfred Dunhill Championship

 
2015 - Charl Schwartzel - Afrika Kusini 
2016 - Brandon Grace - Afrika Kusini 
2018 - David Lipsky - Marekani 
2019 - Pablo Larrazábal - Uhispania 
2020 - Christiaan Bezuidenhout – Afrika Kusini 
 

Shinda na Kombe la Dunia

Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 
 
 
 

Published: 12/07/2022