Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 17
Aston Villa v Liverpool
Villa Park
Birmingham, England
Monday, 26 December 2022
Kick-off is at 20h30
Liverpool na Aston Villa watakabiliana katika mechi ya ligi mnamo Desemba 26.
The Reds walikuwa na kipindi kigumu cha nusu ya kwanza ya msimu huu kwani
walifanikiwa kushinda mechi sita tu kati ya mechi kumi na nne na kutia dosari azma yao
kushindania ubingwa.
Vijana wa Jurgen Klopp waliingia mapumziko ya kombe la dunia wakiwa alama 15
nyuma ya viongozi wa ligi Arsenal na wakiwa katika nafasi ya sita. Lengo ni kuimarisha
matokeo yao ligi itakaporudi Jumatatu Desemba 26.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Wachezaji saba wa kikosi cha kwanza cha Liverpool waliwakilisha mataifa yao katika
mashindano ya kombe la dunia 2022 na Klopp anatarajia wengi wao watakuwa
wamerejea kushiriki mechi dhidi ya Villa.
“Jordan Henderson amerejea tayari. Virgil van Dijk amerudi mazoezini lakini sina hakika
ataweza kucheza,” alisema Klopp.
“Tutaangalia uwezekano wa Hendo (Jordan Henderson) kucheza kama ilivyo kwa Trent
[Alexander-Arnold]. Kikosi hiki kimefanya mazoezi kwa pamoja karibu wiki mbili na
tumepiga hatua.
“Nina imani tutakuwa salama. Kama tunavyofahamu, kuna virusi vinavyosambaa
Uingereza na Ulaya kwa ujumla. Imani yetu tutaepuka virusi hivi na tutakuwa salama.”
Aston Villa walishinda mechi mbili za mwisho za ligi mwezi Novemba dhidi ya
Manchester United (3-1) na 2-1 dhidi ya Brighton na kujiondoa katika balaa la kushuka
daraja.
Ulikuwa ni mwanzo mzuri kwa Unai Emery aliyechukua nafasi ya Steven Gerrard
Novemba 1, baada ya mchezaji huyo wa zamani kuachishwa kazi Oktoba 20 kufuatia
msururu wa matokeo mabaya.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Villa wapo katika nafasi ya kumi na mbili kwenye ligi na Unai Emery amekiri kuwa
ushindi wa mechi mbili mfululizo umewapa motisha wachezaji wake kuelekea msimu wa
sikukuu.
“Wachezaji walihisi kama walikuwa katika nafasi ya mwisho. Ushindi wa mechi mbili
muhimu umetupa motisha na tunatazamia kuimarika zaidi,” alisema raia huyo wa
Uhispania.
“Wachezaji wote wanajiamini na wana motisha. Jambo hili linatokana na matokeo
mazuri. Tulijituma kwa bidii. Najivunia juhudi zao.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Aston Villa - 1
Liverpool - 4
Sare - 0
Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.