Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kuna uwezekano Cameroon itaaga
kombe la dunia 2022 mapema huku Ghana ikipania kisasi dhidi ya Uruguay Ijumaa kwa yaliyotokea 2010.
Mechi za kundi H zitaanza na Ghana kuikabili Uruguay ugani Al Janoub Stadium mjini Al Wakrah na kisha Korea Kusini na Ureno kukabana koo katika uga wa Education City Stadium, Al Rayyan.
The Selecao ya Ureno inaongoza kwa alama sita baada ya kushinda mechi za kwanza mbili. Wanafuatwa katika nafasi ya pili na Black Stars ya Ghana wakiwa na alama tatu baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Taegeuk Warriors Jumatatu.
Korea Kusini na La Celeste ya Uruguay wana alama moja kila mmoja katika nafasi ya tatu na nne mtawalia, huku Uruguay ikipoteza 2-0 dhidi ya Ureno Jumatatu.
Ghana watakuwa na uchu wa kulipiza kisasi dhidi ya Uruguay kutokana na matokeo ya mechi ya robo fainali ya kombe la dunia mwaka 2010 ambapo Luis Suarez alizuia mpira makusudi kwa mikono na kunyima taifa hilo la Afrika Magharibi ushindi wa muda wa ziada. Asamoah Gyan alishindwa kufunga penalti na baadaye Ghana kushindwa katika matuta ya penalti.
Kocha mkuu wa Black Stars Otto Addo anakiri kuwa timu ya Uruguay itakuwa hatari kubwa lakini ana imani kikosi chake kina uwezo wa kuwatuliza Uruguay watakapokutana.
"Haitakuwa rahisi lakini nina imani tuna uwezo wa kushinda mechi hii,” alisema Addo. “Wana washambuliaji wazuri, wachezaji wengi walio na uzoefu na kikosi kizuri.
"Itakuwa mechi ngumu kama mechi nyingine yoyote. Tulisema kabla ya shindano hili mechi yoyote haitakuwa rahisi na tutahitaji kujituma zaidi ili kushinda mechi hizi.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Ureno wapo katika nafasi nzuri kushinda kundi hilo kwa kushinda mechi zote watakapokutana na Korea Kusini. Cho Gue Song aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Korea Kusini kufunga zaidi ya goli moja katika mechi ya kombe la dunia alipofunga magoli mawili dhidi ya Ghana japo haikutosha kuwapa vijana wa Paulo Bento ushindi wa kwanza.
Kundi G linaongozwa na Brazili wakiwa na alama sita wakifuatiwa na Uswizi na alama tatu huku Cameroon na Serbia wakiwa na alama moja kila mmoja.
The Indomitable Lions ya Cameroon watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Brazil ugani Lusail Iconic Stadium, Lusail ili kuweka matumaini yao kusailia katika mashindano haya hai.
Timu hiyo chini ya ukufunzi wa Rigobert Song ilipoteza mechi ya kwanza 1-0 dhidi ya Uswizi kabla ya kulazimisha sare ya 3-3 dhidi Serbia siku ya Jumatatu.
Song anasisitiza kuwa taifa hilo linazidi kuimarika kila uchao na imani ipo wana uwezo wa kupata ushindi dhidi ya Selecao ya Brazil ambao hadi kufikia sasa hawajaruhusu goli hata moja katika shindano hili.
"Cha muhimu tulionyesha juhudi kubwa na uwezo wa kupamba,” alisema Song. “Tulipambana vizuri baada ya kuwa chini kwa magoli 3-1 na kurudi mchezoni. Tunazidi kuimarika.
"Uwezo tunao wa kushinda Brazil. Tuna imani na uwezo wetu. Hatukuja hapa kushiriki tu. Timu hii bado ina mengi ya kuchangia katika shindano hili.”
Uswizi itamenyana na Serbia ugani Stadium 974 mjini Doha wakiwa na lengo la kuingia hatua ya muondoano katika mashindano matatu mfululizo.
Chini ya mwalimu Murat Yakin, timu hiyo ilianza mashindano haya kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Cameroon na kupoteza 1-0 dhidi ya Brazil, bao lililofungwa na Casemiro kunako dakika ya 83.
The Eagles ya Serbia itahitaji ushindi mkubwa dhidi ya Uswizi ili kufuzu hatua ya muondoano kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 baada ya kuruhusu magoli matano kwenye mechi mbili za kwanza.
Ratiba ya mechi za kombe dunia Ijumaa Desemba 2
6:00pm: Korea Kusini v Ureno
6:00pm: Ghana v Uruguay
10:00pm: Cameroon v Brazil
10:00pm: Serbia v Uswizi
Shinda na Kombe la Dunia
Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.