Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 National Basketball Association (NBA) season
Regular Season
Boston Celtics v Miami Heat
TD Garden
Boston, USA
Saturday, 3 December 2022
03h30
Boston Celtics watamenyana na Miami Heat katika mechi ya ligi ya kikapu,
National Basketball Association (NBA) mnamo Desemba 3.
Hii itakuwa ni mara ya 131 baina ya timu hizi kukutana katika mechi za msimu wa kawaida tangu mwaka 1988, wakati The Heat ilianzishwa.
The Celtics wamekuwa wakionyesha ubabe mara nyingi wanapokutana na the Heat kwani wameshinda mara 79 dhidi ya mara 51 kwa faida ya the Heat.
Mara ya mwisho katika ligi walikutana mnamo Oktoba 22 2022 kwenye mchezo uliochezewa ukumbini FTX Arena, Miami, Florida, Biscayne Bay.
The Celtics walipata ushindi wa 111-104 ambapo Jayson Tatum alionyesha mchezo mzuri na kuchangia vikapu 29, kusaidia kupatikana vikapu 4 huku Jaylen Brown akichangia vikapu 28 na kusaidia kupatikana vikapu 3.
The Celtics wanaongoza katika jedwali la michezo ya Eastern Conference baada ya kuandikisha ushindi wa mechi 17 na kushindwa mara 4 katika mechi 21.
Kwingineko the Heat wapo katika nafasi ya 10 katika michezo ya Eastern Conference baada ya kuandikisha ushindi wa mechi 10 na kupoteza mechi 11 katika mechi 21.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mkufunzi wa muda wa Celtics Joe Mazzulla alionyesha kuridhishwa na Blake Griffin katika ushindi wa timu hiyo wa 140-105 dhidi ya Charlotte Hornets Jumanne Novemba 29.
“Ni mtu muungwana,” alisema Mazzulla ambaye alitajwa kuwa kocha wa muda wa Celtics baada ya Ime Udoka kusimamishwa kwa muda uliosalia wa msimu miezi miwili iliyopita.
“Amekuwa wa msaada mkubwa kwenye timu ndani na nje ya uwanja. Anajituma sana, ana kasi na anashirikiana vizuri na wachezaji wenzake.
"Vile vile nimemshukuru kwa uadilifu katika kazi yake na kwa kuwa tayari muda wote anapohitajika na timu. Msimu ni mrefu na tutahitaji sifa hizi kwa kweli.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za NBA
Mechi - 5
Celtics - 4
Heat -1
Ratiba ya mechi za NBA - 3-4 Desemba
Desemba 3 Jumamosi
03:00am - Charlotte Hornets v Washington Wizards
03:30am - Atlanta Hawks v Denver Nuggets
03:30am - Boston Celtics v Miami Heat
03:30am - Brooklyn Nets v Toronto Raptors
03:30am - Cleveland Cavaliers v Orlando Magic
03:30am - Milwaukee Bucks v Los Angeles Lakers
04:00am - Memphis Grizzlies v Philadelphia 76ers
04:00am - San Antonio Spurs v New Orleans Pelicans
05:00am - Phoenix Suns v Houston Rockets
05:00am - Utah Jazz v Indiana Pacers
06:00am - Golden State Warriors v Chicago Bulls
20:30pm - New York Knicks v Dallas Mavericks
00:00am - Los Angeles Clippers v Sacramento Kings
Desemba 4 Jumapili
02:00am - Charlotte Hornets v Milwaukee Bucks
04:00am - Minnesota Timberwolves v Oklahoma City Thunder
04:00am - Toronto Raptors v Orlando Magic
04:30am - Golden State Warriors v Houston Rockets
05:00am - Utah Jazz v Portland Trail Blazers
23:30pm - New Orleans Pelicans v Denver Nuggets
24:00pm - San Antonio Spurs vs Phoenix Suns
Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.