76ers na nia ya ushindi dhidi ya Lakers


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 National Basketball Association (NBA) season

Regular Season

Philadelphia 76ers v Los Angeles Lakers 

Wells Fargo Center
Philadelphia, USA
Saturday, 10 December 2022
03h30  
 
Philadelphia 76ers itamenyana na Los Angeles Lakers katika mechi ya ligi ya National Basketball Association (NBA) mnamo Desemba 10.
 
Hii itakuwa ni mara ya 288 timu hizi kukutana tangu mwaka 1950 na ni moja kati ya mechi kali kabisa baina ya timu katika historia ya NBA.
 
The Lakers wameshinda mechi 146 baina ya timu hizi ukilinganisha na mara 141 kwa faida ya 76ers 141.

Tobias HarrisHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Timu hizi zilikutana mara ya mwisho mnamo Machi 24 2022 kwenye ukumbi wa Crypto.com Arena mjini Los Angeles ambapo 76ers waliibuka na ushindi.
 
Kwa ujumla, Joel Embiid alichangia alama 40 na James Harden alama 24 huku 76ers wakiibuka na ushindi wa 126-121 dhidi ya Lakers licha ya kukosa huduma za LeBron James.
 
76ers wanashikilia nafasi ya sita kwenye michezo ya Eastern Conference baada ya kushinda mechi 12 na kushindwa mechi 11 katika mechi 23.
 
Kwengineko Lakers wanashikilia nafasi ya 12 kwenye michezo ya Western Conference baada ya kushinda mechi 10 na kupoteza mechi 12 katika mechi 22.

Doc Rivers - 76ers coach
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mkufunzi wa 76ers Doc Rivers amedokeza kuwa mchezaji Shake Milton atakuwa akicheza mara kwa mara ukizingatia Embiid, Harden na Tyrese Maxey wanauguza majeraha.
 
“Sio kila mchezaji atapata nafasi ya kucheza lakini baadhi watapata nafasi hiyo na Shake Milton atakuwa mmoja wao,” alisema River.
 
“Kuna ushindani mkubwa wa nafasi za kucheza katika kikosi na Shake ameonyesha kuwa anastahili kucheza. Natarajia ataendelea kuonyesha juhudi hizo. Ana mchango mkubwa hata kwa muda mfupi.
 
“Kuna wachezaji wanaopata muda mwingi na wanafanya vizuri. Wengine wanapata muda mchache lakini hawaonyeshi juhudi. Shake ana uwezo mkubwa na atatusaidia sana.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho NBA.

Mechi - 5
76ers - 4
Lakers - 1
 

Ratiba ya mechi za NBA- 10-11 Desemba 


Desemba 10 Jumamosi

03:00am - Charlotte Hornets v New York Knicks
03:00am - Indiana Pacers v Washington Wizards
03:00am - Orlando Magic v Toronto Raptors
03:30am - Brooklyn Nets v Atlanta Hawks
03:30am - Cleveland Cavaliers v Sacramento Kings
03:30am - Philadelphia 76ers v Los Angeles Lakers
04:00am - Memphis Grizzlies v Detroit Pistons
04:30am - New Orleans Pelicans v Phoenix Suns
05:00am - Utah Jazz v Minnesota Timberwolves
06:00am - Dallas Mavericks v Milwaukee Bucks

Desemba 11 Jumapili

01:00 - Miami Heat v San Antonio Spurs
03:00am - Indiana Pacers v Brooklyn Nets
03:00am - Washington Wizards v Los Angeles Clippers
03:30am - Cleveland Cavaliers v Oklahoma City Thunder
04:00am - Chicago Bulls v Dallas Mavericks
04:30am - Golden State Warriors v Boston Celtics
05:00am - Denver Nuggets v Utah Jazz
06:00am - Portland Trail Blazers v Minnesota Timberwolves
23:30pm - New Orleans Pelicans v Phoenix Suns
 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 12/07/2022