Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Premier League
England
13 August 2021 - 22 May 2022
Mbio kuwania taji la ufungaji bora katika
ligi ya premier zinaendelea kupamba moto huku wachezaji wengi wakiwania tuzo hilo.
Betway wanaangazia wachezaji watatu wanaowania tuzo hilo.
Mreno huyu amekuwa na msimu wa kufana na wekundu wa Anfield akiwa amefunga magoli nane kwenye mechi kumi na nane. Kwa sasa yupo nafasi ya tatu katika chati ya wafungaji bora wa ligi.
Ni mshambuliaji mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kufunga magoli. Jota alifunga magoli matatu katika mechi tatu mwezi Novemba na kuteuliwa kuwania tuzo la mchezaji bora wa ligi mwezi huo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anawania tuzo hilo pamoja na washambuliaji mahiri nchini Uingereza akiwemo Mohamed Salah na Jamie Vardy.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mshambuliaji huyo mkongwe kutoka England anaonekana kurejea katika ubora wake wa kufunga magoli uliompelekea kushinda tuzo hilo msimu 2019/20.
Vardy anayejulikana kwa hari yake, kasi kubwa na uwezo wa kushambulia, anashakilia nafasi ya pili katika chati ya ufungaji akiwa na magoli tisa kwenye mechi kumi na tano.
Vardy alifunga magoli 23 aliposhinda tuzo hilo akimpiku Salah lakini kwa sasa wachezaji hao wako sako kwa bako msimu huu.
Nyota huyo kutoka Misri hashikiki msimu huu huku akifunga magoli 13 kwenye mechi 15 na anaongoza chati za ufungaji katika ligi ya premier.
Salah, anayejulikana kwa kasi, uwezo wa kufunga magoli na uwezo wa kuwachenga wapinzani ananuia kushinda tuzo hilo kwa mara ya tatu msimu huu.
Wengi wakimtaja kuwa mchezaji bora duniani kwa sasa, Salah anapigiwa upato kushinda tuzo la msimu huu baada kushinda tuzo hilo msimu 2017/18 na 2018/19.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Natumai mengi zaidi! Lengo langu kwanza ni kushinda taji na klabu; klabu bingwa ulaya, ligi ya premier au zote mbili. Hilo ndilo lengo la kila mmoja,” alisema Salah.
“Ni matokeo mazuri. Kuja hapa na kushinda mechi tukionyesha mchezo mzuri na kufunga magoli manne ni faraja sana. Tumejifunza mengi kutokana na mechi hiyo.
“Kocha wetu alitwambia kuwa watacheza kwa kujituma na kutumia nguvu nyingi,” aliendelea.
“Tusitoke kwenye mbinu zetu na tumiliki mpira na kujaribu kutengeneza nafasi jambo ambalo tulifanya.”
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.