Verstappen afukuzia ushindi wa Abu Dhabi


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021 FIA Formula One World Championship 

2021 Abu Dhabi Grand Prix

Yas Marina Circuit
Abu Dhabi, United Arab Emirates 
Sunday, 12 December 2021
 
Max Verstappen wa Red Bull Racing-Honda atapania kushinda taji la mbio za langalanga mkondo wa Abu Dhabi  mnamo Disemba 12. 
 
Verstappen mwenye umri wa miaka 24 ataelekea katika mbio hizo za mwisho wa msimu wa 2021 akishikilia nafasi ya kwanza katika chati ya madereva sambamba na Lewis Hamilton, wote wakiwa na alama 369.5 
 
Verstappen amekuwa na ushindi mara tisa ndani ya msimu na alichukua nafasi ya pili katika mbio tatu za mwisho huku ushindi wa madereva ukiamuliwa na mbio za mwisho.

Lewis Hamilton
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Hamilton ambaye ndiye bingwa mtetezi alirekodi mzunguko wa kasi zaidi na kuwa mshindi wa awamu ya mbio za Saudi Arabia ambapo alimaliza sekunde 21 mbele ya mpinzani wake mkuu Verstappen. 
 
Valtteri Bottas alimaliza wa tatu katika mbio hizo zilizoandaliwa katika mkondo wa Jeddah Corniche Circuit huku Mercedes ikiimarisha nafasi yake kwa ujumla. 

Valtteri Bottas
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Bottas atamaliza katika nafasi ya tatu bila kujali kama atapata alama zozote au la kule Abu Dhabi kwa sababu Sergio Perez anayeshikilia nafasi ya nne hawezi kumfikia katika msimamo wa jedwali. 
 
Akitoa maoni yake kuhusu mbio hizo za mwisho, Verstappen alisema, “kwa sasa tunatoshana alama na hilo linafurahisha na kuleta mhemko katika mbio na Formula One kwa ujumla. Kila kitu kitaamuliwa na mbio hizo kwa hivyo natumai tutakuwa na wikendi ya kufana.”
 

Matokeo ya mbio za 2021 za mkondo wa Saudi Arabia

 
Mshindi: Lewis Hamilton - Mercedes
Nafasi ya pili: Max Verstappen - Red Bull Racing-Honda
Nafasi ya tatu: Valtteri Bottas - Mercedes

 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 12/09/2021