Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Spanish La Liga
Matchday 16
Real Sociedad v Real Madrid
Estadio de Anoeta
San Sebastian, Spain
Saturday, 4 December 2021
Kick-off is at 23h00
Real Sociedad watakuwa wenyeji wa Real Madrid katika
mechi ya ligi uwanjani Reale Arena, kwa jina lingine Estadio de Anoeta mnano Disemba 4.
Katika mechi ya ligi iliyochezwa Novemba 28, Real Sociedad walipoteza mchezo dhidi RCD Espanyol kwa 1-0.
Hadi kufikia mechi hiyo dhidi ya Espanyol, Sociedad walikuwa hawajapoteza mechi yoyote ya ligi kati ya kumi na tatu zilizopita. Walikuwa wameandikisha ushindi mara nane na kupata sare tano.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Hata hivyo, The White and Blues wamekuwa na rekodi nzuri wakiwa nyumbani. Katika mechi kumi za ligi zilizopita, wameshinda mechi saba na kulazimisha sare tatu ugani Reale Arena.
"Tulikuwa na mchezo mzuri katika sekta nyingi za mechi hiyo lakini bahati mbaya matokeo yalitukataa,” meneja wa Real Sociedad Imanol Alguacil alisema baada ya kushindwa na Espanyol.
"Unapotengeneza nafasi na ukakosa kuzitumia kufunga magoli, mpinzani atakuadhibu kama ilivyotokea kwetu. Tunao wachezaji wenye uwezo huo lakini hatukuwa katika ubora wetu.
"Katika nyakati tofauti za mechi tumekuwa tukifanya maamuzi yasiyo sahihi. Pasi tunazotoa hazifiki na hivyo wapinzani wanatuadhibu. Naamini tutafanyia kazi mapungufu hayo na tutaweza kufunga magoli.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwa upande wao, Madrid walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Sevilla katika mechi ya ligi iliyogaragazwa Novemba 28.
Madrid wameshinda mechi tano na kutoa sare moja katika mechi sita za ligi zilizopita.
Vile vile, Madrid wamekuwa na msururu wa matokeo mazuri wakiwa ugenini huku wakiandikisha ushindi mara tatu mfululizo katika mechi tatu zilizopita.
Mara ya mwisho timu hizi kukutana katika mchezo wa ligi ilikuwa Machi 1 2021.
Mechi hiyo iliishia sare ya 1-1na ilichezewa katika uwanja wa kufanyia mazoezi wa Real Madrid, Estadio Alfredo Di Stefano.
Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho za ligi
Mechi - 5
Sociedad - 1
Madrid - 2
Sare - 2
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.