Sevilla kuialika Atletico katika mechi kubwa ya La liga


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 18

Sevilla FC v Atletico Madrid 

Estadio Ramón Sánchez Pizjuán
Sevilla, Spain 
Saturday, 18 December 2021
Kick-off is at 23h00  

Sevilla FC watakuwa wenyeji wa Atletico Madrid katika mechi ya La liga ugani Estadio Ramón Sánchez Pizjuán  mnamo Disemba 18.
 
Katika mechi iliyochezwa Disemba 11, Sevilla waliibuka na ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Athletic Bilbao.
 
Sevilla wameandikisha ushindi mara mbili mfululizo katika mechi mbili za mwisho za ligi.

Julen Lopetegui
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vile vile, Sevilla hawajapoteza mechi yoyote ya ligi nyumbani kati ya tisa za mwisho baada ya kuandikisha ushindi katika mechi nane na sare moja.
 
"Ni ushindi wa kufurahia kwa sababu sio sehemu rahisi kupata matokeo na hatujapata ushindi mara nyingi miaka ya hivi karibuni,” alisema meneja wa Sevilla Julen Lopetegui walipoishinda Bilbao.
 
"Tumekuwa na changamoto si haba wiki hii ikiwa ni pamoja na kuondolewa katika ligi ya mabingwa, kupata majeraha na uchovu mwingi. Wapinzani wetu walijiandaa vya kutosha kwa ajili ya mechi hii lakini tumejituma zaidi.
 
"Wengefunga lakini haikutokea. Ni jambo la kawaida ambalo pia sisi tumepitia katika mechi nyingine. Tulicheza vizuri kipindi cha pili na tumefanikiwa kupata alama tatu muhimu na zilitufaa.”

Rodrigo De Paul
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

kwengineko, Atletico walichezea kipigo cha 2-0 wakiwa ugenini kutoka kwa wapinzani wao wa jadi Real Madrid katika mechi iliyochezwa Disemba 12.
 
Kwa sasa Atletico Madrid wamepoteza mechi mbili za ligi mfululizo.

Kabla ya kipigo cha Real Madrid, Atletico walikuwa na mechi tatu za ligi bila kushindwa ugenini huku wakirekodi ushindi mmoja na sare mbili.
 
Mechi ya mwisho baina ya Sevilla na Atletico ilikuwa Aprili 4 2021.

Sevilla ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Atletico uwanjani Estadio Ramón Sánchez Pizjuán.
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Sevilla - 1
Atletico - 1
Sare - 3


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 12/14/2021