Real na Atletico kutoana kijasho katika Debi ya Madrid


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 17

Real Madrid v Atletico Madrid 

Estadio Santiago Bernabéu
Madrid, Spain 
Sunday, 12 December 2021
Kick-off is at 23h00  

Real Madrid watakuwa wenyeji wa Atletico Madrid katika mechi ya ligi kuu ya Uhispania Disemba 12 ugani Estadio Santiago Bernabéu.

Wakiwa ugenini, Real Madrid waliishinda Real Sociedad kwa 2-0 katika mchezo wa ligi uliopita wa tarehe 4 Disemba.
 
Katika mechi nane za ligi zilizopita, Real Madrid wamekuwa na matokeo mazuri huku wakiandikisha ushinda mara saba na kupata sare mara moja.

Luka Modric
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Vile vile, Real Madrid hawajapoteza mechi yoyote nyumbani kati ya kumi na saba za ligi zilizopita huku wapata ushindi mara 12 na sare 5.
 
“Wachezaji wanajivunia sana kwa mchezo tulioonyesha jioni ya leo. Kwa ujumla ulikuwa mchezo mzuri,” alisema kiungo wa Madrid Luka Modric baada ya ushindi dhidi ya Sociedad.
 
"Tulianza mechi vizuri sana na kuwachanganya Real Sociedad kutotumia mbinu zao. Tulifahamu utakuwa mchezo mgumu sana katika uwanja wao wa nyumbani lakini tulijituma na kuonyesha mchezo mzuri tangu mwanzo na kufunga magoli mawili.”
 
“Tunafurahishwa na jinsi msimu wetu unavyoenda na jinsi tunavyocheza. Ni lazima tuendelee hivyo hivyo. Ushindi hupatikana unavyohusika katika mechi kama tulivyofanya jioni ya leo. Kikosi kizima kiko vizuri na mazoezi kama inavyoshuhudiwa na matokeo yetu.”

Yannick Carrasco
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

katika hali ya kushangaza, Atletico wakiwa nyumbani walipigwa na Real Mallorca 2-1 katika mechi ya ligi mnamo Disemba 4.
 
Hadi kufikia mechi hiyo, Atletico walikuwa hawajashindwa katika mechi saba za ligi zilizopita huku wakiandikisha ushindi mara nne na kupata sare tatu.
 
Hata hivyo, Atletico hawajapoteza mechi yoyote ya ligi kati ya tatu za mwisho walizocheza ugenini. Wamepata sare mara mbili mfululizo na ushindi mara moja.
 
Mara ya mwisho timu hizi kukutana katika ligi ilikuwa Machi 7 2021.
 
Mechi hiyo iliishia sare ya 1-1 ugani Estadio Metropolitano iliyobadilisha jina kuwa Wanda Metropolitano kwa sababu za ufadhili.

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5 
Real - 3
Atletico - 0
Sare - 2


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 
 

Published: 12/08/2021