Miamba wa England, Chelsea na Liverpool kukabana koo


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 21 of 38

Chelsea vs Liverpool

Stamford Bridge 
London, England
Sunday, 02 January 2022
Kick-off is at 19:30  

Chelsea na Liverpool watakabana koo katika mechi ya ligi mnamo jumapili januari 2 2022. 

Jurgen Klopp
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Timu hizi zinatazamia kuendelea kuishinikiza Man city ambao ndio viongozi wa ligi, wote wakiwa wanapania kushinda taji hilo. 
 
Chelsea imekuwa miongoni mwa timu zilizotibuliwa na janga jipya la corona, Omicron. Hitilafu hizo zimepelekea timu hiyo kupata sare mbili na sasa wameachwa na viongozi Man City na alama sita.
 
Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel anashangaa kwa nini mechi yao ya tarehe 26 aijahairishwa ikizingatiwa mechi ya Liverpool ya siku hiyo imefanywa hivyo. Tuchel anasema ni hatari kuwaharakisha wachezaji kurudi mchezoni baada ya majeraha kwani kuna wachezaji wachache tu. 
 
"Naelewa vizuri kila mtu anaposema kuna tuna wachezaji 14 lakini ukiangalia kwa undani ; Trevoh Chalobah amefanya mazoezi mara mbili tangu atoke majeraha, Mateo Kovacic mara moja na Ngolo Kante mara moja. 
 
"Tunahatarisha Maisha ya wachezaji kwa kuwachezesha mechi nyingi kupita kiasi achia mbali maambukizi ya Corona,” Tuchel alisema mwezi Disemba. 
 
Jurgen Klopp amekashifu vikali ratiba ya mechi msimu huu wa sikukuu huku timu yake ikipangiwa kucheza mechi mbili kipindi cha siku tatu kabla ya mechi ya tarehe 26 dhidi ya Leeds Kuahirishwa. 
 
The Reds waliingia kipindi cha Krismasi wakiwa katika msururu wa mechi saba bila kushindwa, wakiwa katika nafasi ya bila nyuma ya City kwa alama tatu.
 
"Sina tatizo na mechi za krismasiI. Hakuna anayehitaji kuzifuta lakini kucheza tarehe 26 na 28 haiwezekani. Ni mchezo mbaya wanaoendelea kuufanya. Hakuna shida kucheza tarehe 26 na 29,” alisema Klopp. 
 
"Watu wanaweza kusema malipo yao ni mazuri lakini hili halihusiani kabisa. Kucheza tarehe 26 na 29 inawezekana lakini ni hatari kwa wachezaji. Kila timu inatarajia kushinda. 
 
"Kuna timu mbili zenye wachezaji wote katika hali nzuri kiafya. Chelsea sio moja yao kwa sasa. Kuna uwezekano City wana kikosi cha kucheza mechi mbili na kumaliza ligi lakini timu nyingine hazina uwezo huo. Hilo ndilo tatizo,” aliongeza. 
 
Chelsea na Liverpool wataathirika sio tu na Corona bali pia na shindano la AFCON litakalohitaji Mo Salah, Sadio Mane, Naby Keita wote wa Liverpool na Chelsea itakosa huduma za Edouard Mendy atakayekuwa nje kwa muda wa wiki sita. Chelsea watakuwa na kiungo wa Morocco Hakim Ziyech baada ya kuachwa nje ya kikosi cha Morocco.

Mohamed Salah
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Mchezo wa kwanza msimu huu baina ya timu hizi mbili uliishia kwa sare ya 1-1 ugani Anfield. Kai Havertz alikuwa mfungaji wa Chelsea kabla ya Mo Sahah kusawazisha kupitia penalty baada ya Reece James wa Chelsea kuonyeshwa kadi nyekundu kabla ya kipindi cha kwanza. 
 

Matokeo baina ya Chelsea na Liverpool 

 
Mechi: 179
Chelsea: 61
Liverpool: 76
Sare: 42
 

Ratiba ya mechi za EPL, mchezo wa 21

 
Jumamosi 01 Januari 01 
 
15:30 - Arsenal vs Manchester City 
18:00 - Leicester City vs Norwich City 
18:00 - Watford vs Tottenham Hotspur 
20:30 - Crystal Palace vs West Ham United 
 
Jumapili Januari 02
 
17:00 - Brentford vs Aston Villa 
17:00 - Southampton vs Newcastle United 
17:00 - Leeds United vs Burnley 
17:00 - Everton vs Brighton & Hove Albion 
19:30 - Chelsea vs Liverpool 
 
Jumatatu Januari 03
 
20:30 - Manchester United vs Wolverhampton Wanderers 


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 12/28/2021