Mashindano ya Hero World Challenge 2021 Kung’oa nanga


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021 Hero World Challenge 

US PGA Tour 

Albany Golf Club 
New Providence
The Bahamas
2-5 December 2021  
 
Mashindano ya gofu ya Hero World Challenge ya 2021 yanatazamiwa kufanyika kati ya Disemba 2 na 5 Albany Golf Club, New Providence kule Bahamas. 
 
Haya yatakuwa Makala ya 22 ya shindano hili ambalo huandaliwa kila Disemba na Tiger Woods. Mwaka 2020 halikufanyika kutokana na janga la COVID-19. 
 
Shindano hili ni sehemu ya PGA tour ingawaje hakuna alama wala hela za kushindania kwa sababu sio shindano rasmi. 

Justin Thomas
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Henrik Stenson ndiye bingwa mtetezi wa Hero World Challenge baada ya kushinda shindano lililoandaliwa mwaka 2019. 
 
Nyota huyo kutoka Sweden atakuwa miongoni mwa wachezaji wachache watakaoshiriki huku akitazamia kutetea taji hilo. 
 
Baadhi ya mabingwa wa zamani wa FedExCup watakaoshiriki ni pamoja na  Rory McIlroy (2016, ’19), Jordan Spieth (2015), Justin Thomas (2017) na Justin Rose (2018) 
 
Collin Morikawa ambaye ni bingwa wa DP World tour pamoja na Webb Simpson mshindi wa zamani wa US Open watashiriki pia. 

Jordan Spieth
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
“Washiriki wote wa mwaka huu wa 2021 wanafurahi sana kuwa sehemu ya Hero World Challenge,” alisema mkurugenzi wa shindano hili Mike Antolini. 
 
“Tunafurahi shindano hili kuandaliwa tena Albany, Bahamas”.
 
Woods anashikilia rekodi ya kuwa mshindi mwenye mataji mengi ya Hero World Challenge huku akiwa na mataji matano. 
 
Woods mwenye mataji 15 ya mashindano makubwa hawezi kushiriki kwa sababu anazidi kuuguza majeraha aliyopata kutokana na ajali ya gari iliyotokea Februari,huku tarehe ya kurudi kwenye mashindano ikiwa haijulikani. 
 
Davis Love III na Graeme McDowell wameshinda shindano hili la Hero World Challenge mara mbili kila mmoja. 
 

Washindi watano wa mwisho wa shindano la Hero World Challenge

 
2015 - Bubba Watson – Marekani 
2016 - Hideki Matsuyama - Japan
2017 - Rickie Fowler- Marekani
2018 - Jon Rahm - Uhispania
2019 - Henrik Stenson - Sweden 
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 12/02/2021