Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 English Premier League
Matchday 19
Manchester City v Leicester City
Etihad Stadium
Manchester, England
Sunday, 26 December 2021
Kick-off is at 18h00
Manchester City wataialika Leicester city ugani Etihad Disemba 26 huku wakinuia kuendeleza ubabe wao katika ligi.
Vijana hao wa Pep Guardiola wameandikisha msururu wa matokeo mazuri katika
mechi nane na sasa wanaongoza jedwali wakiwa alama tatu mbele ya Liverpool.
Ushindi wa 4-0 dhidi ya Newcastle Disemba 19 ulifikisha magoli yaliyofungwa na City 44, Liverpool ikiwazidi kwa mabao 6.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Ushindi huo ulipelekea City kuweka rekodi mbili; ushindi wa 34 wa 2021 na ushindi wa 18 ugenini huku Guardiola akiwasifia sana vijana wake kwa mafanikio hayo.
"Ushindi wa mechi nyingi mfululizo unaashiria uchezaji wetu mzuri na sio kwa msimuu huu tu bali kutoka miaka minne au mitano iliyopita,” alisema Guardiola.
'Ni rekodi ya muda murefu. Sio rahisi kupatikana na tunaelewa hilo. Rekodi zote siku moja zitavunjwa na ni vizuri. Ni ishara kuwa wachezaji wetu wanacheza vizuri.’
Kwengineko, Leicester hawajawa na matokeo mazuri sana huku mara ya mwisho kushinda mechi mfululizo ikiwa ni Oktoba.
Leicester waliitwanga Newcastle 4-0 Disemba 12 baada ya kushindwa na Aston Villa na kabla ya sare ya 2-2 Southampton.
Leicester wanashikilia nafasi ya tisa katika jedwali la ligi na wana safari ndefu ya kufika nne bora.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Rogers anasema wakati huu wa Krismasi umekuwa na changamoto ambazo pia zimechangiwa na uwepo wa visa vingi vya covid.
"Ni mechi nyingi. Ratiba ambayo sio rahisi hasa unapokuwa na wachezaji majeruhi,” alisema.
"Tumekuwa na majeruhi wengi. Ni changamoto kwetu. Tunaheshimu mashindano haya na tutaendelea kupambana.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za premier
Mechi - 5
Man City - 4
Leicester - 1
Sare - 0
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.