Madrid dhidi ya Inter kuamua mshindi wa kundi D


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 UEFA Champions League 

Group D

Real Madrid v Inter Milan 

Santiago Bernabéu, Madrid
Madrid, Spain 
Tuesday, 7 December 2021
Kick-Off 23h00  
 
Real Madrid wataialika Inter Milan Disemba 7 katika mechi ya ligi klabu bingwa barani ulaya kundi D.
 
Miamba hao wa Uhispania walipata ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya mabingwa wa ligi ya Moldova Sheriff Tiraspol iliyochezwa Novemba 24.
 
Kufuatia ushindi huo, Madrid wameshinda mechi tatu mfululizo za shindano hili katika mechi tatu za mwisho.

Carlo Ancelotti
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Novemba 3, Madrid waliishinda Shakhter Donestsk ya Ukraine na kuvunja msururu wa mechi mbili za nyumbani bila ushindi.
 
“Nafurahia tunavyocheza. Inaonyesha tuko katika mkondo mzuri,” alisema Carlo Ancelotti, meneja wa Real Madrid baada ya kuwashinda Sherrif.
 
“Kikosi kizima kiko vizuri. Wachezaji wetu ni wazima kiafya. Tunatazamia kumaliza mechi za makundi kama tulivyoanza; kwa ushindi na kuongoza kundi hilo. Tulikuwa na mchezo mzuri tangu mwanzo.
 
"Walituficha mpira katika nyakati za kwanza lakini baada ya muda tuliwadhibiti. Tulicheza vizuri hadi mwisho mwisho na timu nzima ilijituma.”

Lautaro Martinez
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Katika mchezo wao wa mwisho nyumbani, Inter walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Donetsk Novemba 24.
 
Mabingwa hao wa ligi ya Italia hawajapoteza mechi yoyote ya UEFA kati ya nne zilizopita huku wakiambulia ushindi katika mechi tatu na kupata sare moja.
 
Vile vile, Inter hawajapoteza mechi yoyote ugenini za shindano hili katika mechi tatu zilizopita huku wakiambulia ushindi mara mbili na sare moja.
 
Mara ya mwisho Madrid kuialika Inter katika mechi rasmi ilikuwa Novemba 3 2020.
 
Katika mchezo wa kundi B uliochezewa Estadio Santiago Bernabéu, Madrid alipata ushindi wa 3-2 dhidi ya Inter. 
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi rasmi.

Mechi - 12
Madrid - 6
Inter - 5
Sare - 1


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 12/06/2021