Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 English Premier League
Matchday 16
Liverpool v Aston Villa
Anfield
Liverpool, England
Saturday, 11 December 2021
Kick-off is at 18h00
Liverpool wataialika Aston Villa ugani Anfield katika juhudi zao za kupigania
ubingwa wa ligi mnamo Disemba 11.
Mabingwa hao wa msimu 2019/20 walikwea hadi nafasi ya pili baada ya kupata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Wolves katika mechi ya ligi iliyochezwa tarehe 4 Disemba, Divock Origi akifunga goli dakika ya 94.
Ushindi huo wa nne mfululizo unaipeleka Liverpool katika nafasi ya pili alama moja nyuma ya Manchester City na alama moja mbele ya Chelsea wanaochukua nafasi ya tatu.
Origi amecheza mechi tatu msimu huu na zote akiwa mchezaji wa akiba na Klopp amemsifia mchezaji huyo baada ya kufunga goli hilo muhimu sana kwa majogoo wa Merseyside.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Anawaza kuimarika kila siku, huo ndio ukweli na talanta yake ipo wazi,” alisema kocha huyo mjerumani.
"Ana uwezo kwenye mguu wa kulia na kushoto. Ufundi wake ni wa hali ya juu na anaweza kugeuka upesi sana. Uwezo wake kwenye mipira ya kichwa sote tunaujua. Mchezo wake kwa ujumla unafurahisha.
"Ni jambo zuri sana kuwa sehemu ya kikosi hiki na timu hii kwani kuna mambo mabaya zaidi ya kuwa mchezaji wa akiba mara kwa mara. Ni vizuri ana uwezo mkubwa na alionyesha hili wikendi.”
Steven Gerrard atarejea ugani Anfiled kwa mara ya kwanza tangu alipoichezea klabu hiyo mara ya mwisho mwaka 2015.
Gerrard mwenye umri wa miaka 41 aliichezea klabu hiyo mara 701 katika mashindano yote na sasa amekuwa na mwanzo mzuri kama kocha wa klabu ya Aston Villa.
Mechi yake ya kwanza kama kocha wa Villa ilikuwa na ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion na kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Crystal Palace, 2-1 dhidi ya Leicester na kupoteza 2-1 dhidi ya Manchester City.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Aston Villa wana alama 19, alama 9 juu ya nafasi za kushushwa daraja na mkufunzi huyu ana matumaini ya kufikia nafasi ya kucheza mechi ya Europa.
"Nataka tuwe timu yenye kujiamini,” alisema. “Ni muhimu kuwa jinsi ya kuboreka na kuimarika tukiendelea mbele.
"Ushindi dhidi ya Leicester ni ushindi mkubwa kwa sababu unatupeleka katika nafasi ya kumi bora. Tunazo mechi dhidi ya Wolves na Brighton mbele yet una tunatarajia kupata ushindi.”
Liverpool walishinda mechi ya mkondo wa pili wa msimu uliopita kwa 2-1 baada ya kupoteza mechi ya mkondo wa kwanza wa msimu huo dhidi ya Aston Villa kwa 7-2.
Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Liverpool - 4
Aston Villa - 1
Sare - 0
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.