Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 English Premier League
Matchday 15 of 38
Everton vs Arsenal
Goodison Park
Liverpool, England
Monday, 06 December 2021
Kick-off is at 23:00
Arsenal watanuia kutonesha zaidi kidonda cha Everton katika
mechi za ligi msimu huu watakapokutana ugani Goodson Park Jumatatu jioni.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
The Toffees watacheza na Liverpool kabla ya kuialika Arsenal katika juhudi za kutafuta ushindi baada ya kwenda mechi saba bila ushindi wowote huku shinikizo likizidi kwa kocha Rafa Benitez.
"Sio mashabiki tu wasiwasi, hata sisi wenyewe tuna wasiwasi kwa sababu hatujapata matokeo mazuri,” alisema Benitez baada ya kushindwa 1-0 na Brentford.
"Ukweli ni kwamba wachezaji wanafanya kila juhudi uwanjani, wanaonyesha umoja uwanjani na tunapambana kila dakika. Mashabiki wana haki ya kuwa na wasiwasi lakini bidii yetu uwanjani sio ya kutilia shaka.
"Ni imani yangu tutaanza kufunga magoli na kuandikisha matokeo mazuri,” aliongeza.
Arsenal waliandikisha ushindi wa 2-0 dhidi na Newcastle united kabla ya kukutana na Manchester United na Everton siku chache zijazo.
Baada ya mwanzo mbaya wa msimu huu, The Gunners wamekwea hadi nafasi ya tano baada ya msururu wa matokeo mazuri chini ya ukufunzi wa Mikel Arteta.
"Tumejitahidi sana kupata alama hizi hasa baada ya kupoteza mechi wikendi iliyopita. Inafurahisha. Ni sharti utafute mbini za kushinda. Kwa ujumla tumefanya vizuri,” alisema Arteta kufuatia ushindi dhidi ya Newcastle united.
"Ilitubidi tuwe na subira. Mtiririko wa mchezo lazima uwepo. Kipindi cha pili tulifanya hivyo na tukaanza kutengeneza nafasi na ndipo tukafunga mabao.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Msimu uliopita, Everton walishinda mechi zote mbili dhidi ya Arsenal na kuondoka na alama zote sita. Mechi ya kwanza walishinda 2-1 wakiwa nyumbani na kisha wakapata ushindi wa 1-0 ugani Emirates.
Takwimu baina ya Everton na Arsenal katika ligi.
Mechi: 204
Everton: 59
Arsenal: 102
Sare: 43
Ratiba ya mechi za EPL, Mchezo wa 15.
04 December 04, Jumamosi
15:30 - West Ham United vs Chelsea
18:00 - Newcastle United vs Burnley
18:00 - Wolverhampton Wanderers vs Liverpool
18:00 - Southampton vs Brighton & Hove Albion
20:30 - Watford vs Manchester City
December 05, Jumapili
17:00 - Leeds United vs Brentford
17:00 - Manchester United vs Crystal Palace
17:00 - Tottenham Hotspur vs Norwich City
19:30 - Aston Villa vs Leicester City
December 06, Jumatatu
23:00 - Everton vs Arsenal
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.