Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Leonel Ateba ruska kuitumikia klabu hiyo katika
michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukamilika vibali vya kazi pamoja na ITS yake kuwasili.
Nyota huyo huenda akawa katika kikosi cha Simba katika mchezo ujao dhidi ya Fountain Gate FC utakaochezwa Jumapili, Agosti 25, 2024, uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, Dar es Salaam.
Ateba ni usajili wa kocha mkuu wa Simba Fadlu Davids akiutaka uongozi wa timu hiyo kuongeza mshambuliaji na kuchukuwa nafasi ya Freddy Michael ambaye tayari amepewa THANK YOU.
Meneja wa idara ya habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wamekamilisha taratibu zote za vibali vya mshambuliaji wao Ateba na sasa rasmi kucheza mechi.
Amesema mechi ya Tabora United alishindwa kucheza baada ya vibali vyake kutokamilika ikiwemo ITS kutoka klabu USM Alger, tayari imewasili na ruksa nyota huyo kwa mechi zijazo.
“Tumekamilisha taratibu zote za vibali, Ateba sasa ruksa kucheza ligi, hata tukipangiwa mechi leo mshambuliaji huyo yupo tayari kucheza, ni mipango ya kocha Fadlu tu kumtumia,” amesema Ahmed.
Ameongeza kuwa timu hiyo inaendelea na maandalizi, pamoja na kushinda dhidi ya Tabora United, wanahitaji kuwapa muda zaidi wachezaji wao waendelee kutafuta ubora wao .
“Tumesajili Wachezaji bora sana wamefanya makubwa walikotoka, katika hao Wapo walioanzia juu moja kwa moja na wengine wameanzia chini, iko hivyo duniani kote hasa Mchezaji anapotoka timu ndogo kwenda kubwa au kutoka ligi ndogo kwenda kubwa au anapoenda kwenye timu yenye presha kubwa kama yetu Ni jukumu letu kuwavumilia, kuwatia moyo, kusimama nao nyakati zote ili warejeshe kujiamini na kuupata ubora wao,aina ya Wachezaji tuliokua nao nusu yao wakiupata ubora wao basi Mwaka huu utakua Msimu mzuri kwetu,” amesema Ahmed.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.