EPL - Fulham v Liverpool


Hakimiliki ya picha: Getty Images


2023/24 English Premier League
Mchezo wa 34
Fulham v Liverpool
Craven Cottage
London, England
Jumapili, Aprili 21 2024
Muda: Saa 11:30 jioni majira ya Afrika ya Kati.
 
Liverpool wanapania kuimarisha ndoto zao za kushinda taji la ligi kuu England watakapokabiliana na Fulham ugani Craven Cottage Jumapili Aprili 21.
 
Msururu wa mechi nane bila kushindwa wakiwa nyumbani ulifikia kikomo baada ya the Reds kupoteza 1-0 dhidi ya Crystal Palace Anfield Aprili 14 matokeo yaliyopelekea timu hiyo kushuka hadi nafasi ya tatu nyuma ya Arsenal. 
 
Manchester City waliibuka na ushindi mnono wa 5-1 dhidi ya Luton ugani Etihad na kuchukua nafasi ya kwanza ya ligi baada ya the Gunners kupoteza mechi yao dhidi ya Aston Villa 2-0 ugani Emirates Stadium.
 
The Cottagers walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham mnamo Aprili 14 uwanjani London Stadium na kuimarisha nafasi yao ya kumaliza ligi katika nafasi za kwanza kumi kwenye jedwali. 
 
Ulikuwa ni ushindi wa kwanza katika mechi nne za ligi kwa vijana wa Marco Silva ambao wanashikilia nafasi ya 12, alama moja nyuma Wolves walio katika nafasi ya 11 na alama mbili nyuma ya Brighton walio katika nafasi ya 10. 
 
Wolves na Brighton walipoteza alama mbili kila mmoja kwenye mechi zao za mwisho za ligi huku wakitoa sare ya 2-2 dhidi ya Nottingham Forest na 1-1 dhidi ya Burnley mtawalia.
 
Katika habari ya vikosi, mkufunzi Silva ana kikosi kizima. Hana majeruhi au wachezaji wanaotumikia marufuku hivyo basi hatakuwa na tatizo kuchagua wachezaji wataokabiliana na Liverpool kwa mara ya nne msimu huu. Klopp atakosa huduma za mlinzi Joel Matip, Thiago Alcantara na Conor Bradley kwenye mechi hiyo kutokana na majeraha. 
 
Silva alifurahishwa na mchango wa kiungo Andreas Pereira kwenye mechi dhidi ya West Ham ambapo alifunga magoli mawili huku kocha huyo akikiri kuwa wanafanyia majaribio ya mchezaji huyo raia wa Brazil kucheza zaidi kwenye nafasi za ushambuliaji. 
 
"Ameimarika sana tangu amejiunga nasi. Anashambulia sana na kuzuia nafasi za maeneo ya ushambuliaji. Ni jambo ambalo tumekuwa tukilifanyia mazoezi,” alisema raia huyo wa Ureno. 
 
"Nafurahishwa na uchezaji wake na jinsi anavyosaidia kwenye safu ya kushambulia. Goli la kwanza aliamini kuwa mpira ungerudia alipokuwa. Alionyesha utulivu mkubwa katika kufunga goli hilo.
 
"Mchango wake kwenye goli la pili ulikuwa wa kiwango cha juu n ani matunda ya mazoezi tunayofanya kila wakati. Inakuwa rahisi kushika mazoezi haya vizuri iwapo tunachokifanyia kazi kinazaa matunda kwenye mechi. Inawafanya wachezaji kuamini zaidi na hili litamsaidia Andreas.” 

Luis Diaz
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Klopp amewaasa wachezaji wake kurudia mbinu na mtindo wao wa uchezaji wa kuwaweka wapinzani chini ya shinikizo uwanjani, mtindo ambao umepelekea timu hiyo kuogopwa sana duniani huku akikiri kuwa waliachia Palace nafasi na muda kwenye kisanduku chao na kumruhusu Eze kupata goli dakika ya 14. 
 
"Nahisi vibaya sana,” raia huyo wa Ujerumani aliambia kituo cha Sky Sports. “Sina cha kusema kuhusu mchezo huu. Kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri hata kidogo. Tulipoteza imani kutoka mchezo uliopita, dhidi ya Atalanta.
 
"Tuliruhusu goli jepesi sana kutokana na uzembe. Mchezaji wao alikuwa peke yake kabisa kwenye eneo letu la hatari. Huo ni uzembe usio ruhusiwa kwenye mchezo wa soka. Unahitaji kujituma kwa asilimia mia moja. Curtis Jones alikuwa anaonyesha mchezo mzuri lakini safu ya ushambuliaji ilikuwa mbali sana na safu ya kiungo. 
 
"Macca [Alexis Mac Allister] na Wataru [Endo] hawakushirikiana vizuri katika safu ya kiungo. Safu ya ulinzi ilikaa nyuma zaidi vile vile. Hili sio swala la kulaumiana.
 
"Suluhisho ni kuwa na umoja na kucheza kama timu uwanjani. Tulipofikia sasa hivi ni kujituma zaidi dhidi ya wapinzani na tutafanya hivyo.”
 

Takwimu baina ya timu hizi mechi 5 za mwisho za ligi. 

Mechi - 5
Fulham - 1
Liverpool - 2
Sare - 2
 

Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 34:

 
Aprili 20 Jumamosi
 
3:00pm: Luton Town v Brentford
 
3:00pm: Sheffield United v Burnley
 
7:30pm: Wolverhampton Wanderers v Arsenal
 
Aprili 21 Jumapili
 
1:30pm: Everton v Nottingham Forest
 
3:00pm: Aston Villa v Bournemouth
 
3:00pm: Crystal Palace v West Ham United
 
4:30pm: Fulham v Liverpool


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 04/17/2024