Alamy hisa picha
2023/24 Spanish La Liga
Mchezo wa 32
Real Mallorca v Real Madrid
Estadi Mallorca Son Moix
Palma de Mallorca, Spain
Jumamosi, Aprili 13 2024
Muda: Saa 12:30 jioni majira ya Afrika ya Kati.
Real Mallorca watamenyana na Real Madrid kwenye
mechi ya ligi kuu nchini Uhispania mnamo Aprili 13 ugani Estadi Mallorca Son Moix wakiwa na lengo la kuzima ubabe wa Los Blancos.
Matokeo ya hivi karibuni
The Pirates kama wanavyofahamika Mallorca walilazimisha sare ya 0-0 na Valencia CF ugenini Machi 30 na hawajapoteza mchezo wa ligi katika mechi mbili zilizipita.
Vile vile, Mallorca hawajapoteza mchezo wa ligi katika michezo miwili ya mwisho wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi wa mechi mbili mfululizo ugani Estadi Mallorca Son Moix.
Kwingineko, Madrid walifikisha msururu wa mechi 24 za ligi bila kupoteza hata moja walipoibuka na ushindi wa 2-0 nyumbani dhidi ya Athletic Bilbao mnamo Machi 31.
Pia, Los Blancos hawajapoteza mechi ya ligi katika michezo 11 waliyoshiriki ugenini huku wakiandikisha sare nne na kushinda mechi saba.
Vikosi
Martin Valijent ni mchezaji pekee anayekosekana kwenye kikosi cha Mallorca kutokana na jeraha kwa sasa ila timu hiyo haina mchezaji anayetumikia marufuku yoyote.
Madrid vile vile hawana mchezaji anayetumikia adhabu au marufuku ila watakosa huduma za David Alaba na Thibaut Courtois wanaouguza majeraha.
Nukuu
"Ni hali halisi ya mchezo. Ilitokea kwa Real Sociedad vile vile muda mfupi uliopita,” alisema meneja wa Mallorca Javier Aguirre baada ya timu yake kupoteza dhidi ya Bilbao kwenye fainali ya kombe Copa del Rey Aprili 6.
"Mchezo unahitaji bahati wakati mwingine. Leo haikuwa yetu. Sina lolote baya la kusema kuhusu wachezaji hawa. Tuliwazuia na kuwadhibiti Athletic kwa dakika 120 ukizingatia tulipoteza dhidi yao mechi iliyopita.
"Tulicheza mchezo mzuri. Sina sababu ya kuwakashifu wachezaji wangu. Tunasubiri mechi yetu dhidi ya Madrid Jumamosi inayokuja.”
Takwimu baina ya timu hizi
Madrid waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mallorca kwenye mechi ya mwisho ya ligi baina yao iliyoandaliwa ugani 1-0 Estadio Santiago Bernabeu Januari 3 2024.
Los Blancos wameshinda mechi mbili kati ya mechi tatu za mwisho za ligi dhidi ya Mallorca ambao wamefanikiwa kushinda mechi moja.
Ratiba ya mechi za La Liga mchezo wa 31.
Aprili 12 Ijumaa
8:00pm - Real Betis v Celta Vigo
Aprili 13 Jumamosi
1:00pm - Atletico Madrid v Girona FC
3:15pm - Rayo Vallecano v Getafe CF
5:30pm - Real Mallorca v Real Madrid
8:00pm - Cadiz CF v FC Barcelona
Aprili 14 Jumapili
1:00pm - Las Palmas v Sevilla CF
3:15pm - Granada CF v Deportivo Alaves
5:30pm - Athletic Bilbao v Villarreal CF
8:00pm - Real Sociedad v UD Almeria
Aprili 15 Jumatatu
8:00pm - CA Osasuna v Valencia CF
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.