Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 UEFA Champions League
Quarter-finals
First leg
Real Madrid v Chelsea
Estadio Santiago Bernabeu
Manchester, England
Wednesday, 12 April 2023
Kick-off is at 21h00
Chelsea wanatarajia kurejea kwa Frank Lampard kutawapa motisha watakapokutana na Real Madrid kwenye mechi ya robo fainali ya
UEFA mkondo wa kwanza Jumatano Aprili 12 ugani Bernabeu.
Lampard aliyeshinda kombe hilo akiwa mchezaji mwaka 2011-12 alikabidhiwa mikoba ya kufundisha timu Chelsea kwa kantarasi ya muda mfupi hadi mwisho wa msimu huu baada ya Graham Potter kusimamishwa kazi Aprili 6.
Mchezaji huyo wa zamani wa timu hiyo aliongoza Chelsea kufika hatua ya 16 ya shindano hilo msimu 2020-21 lakini akafutwa kazi Januari 25 kutokana na matokeo mabaya ya ligi. Nafasi yake ilitwaliwa na Thomas Tuchel ambaye alishinda shindano la UEFA miezi minne baadaye.
Hili lilikuwa kombe la pili la UEFA kwa Chelsea. Msimu uliofuata, Chelsea iliondolewa kwenye shindano hilo katika hatua ya robo fainali na Real Madrid ambao watakutana katika hatua hiyo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo.
Chelsea iliibuka na ushindi wa ujumla wa 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund kwenye hatua ya muondoano ya UEFA mwezi uliopita japokuwa hawajashinda mechi yoyote ya ligi katika michezo mitatu iliyopita.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Los Blancos ndio mabingwa watetezi wa kombe la UEFA na sasa wanafukuzia taji la 15 la shindano hili. Ni timu pekee kuwai kushinda kombe la European Cup mara tano mfululizo ikiwa ni mwaka 1956, 1957, 1958, 1959 na 1960 na taji la UEFA mara tatu mfululizo; 2016, 2017 na 2018.
Vijana wa Carlo Ancelotti walifuzu robo fainali kwa kuibandua Liverpool katika hatua ya 16 bora kwa jumla ya mabao 6-2.
Dalili zinaashiria kuwa timu hiyo kutoka Uhispania haitoweza kutetea taji la ligi kwani ipo nafasi ya pili, alama 12 nyuma ya viongozi Barcelona. Hata hivyo, inaweza kushinda kombe la Copa del Rey baada ya kuibandua Barcelona na kuingia fainali.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Katika habari ya vikosi, Madrid watamkosa mchezaji Ferland Mendy ambaye anauguza jeraha la misuli. Armando Broja, Thiago Silva (goti) na Cesar Azpilicueta (kichwa) watakosa mechi hiyo kwa upande wa Chelsea.
Ancelotti alizungumzia mafanikio ya kuwachezesha wachezaji wachanga kama vile Vinicius Junior, Eduardo Camavinga na Rodrygo msimu huu kwa pamoja na wazoefu kama Toni Kroos, Luka Modric na Karim Benzema akisema wamefanya vizuri sana.
"Wachezaji hawa wanatengeneza mazingira mazuri hasa kwa sababu ya maarifa na unyenyekevu walionao. Vile vile, unyenyekevu wa wachezaji wazoefu ni muhimu kwa sababu hawana kiburi,” alisema.
"Wachezaji wachanga wanatakiwa kuwa na subira na kufahamu kuwa kuna wachezaji walio na uzoefu mkubwa kwenye kikosi.”
Lampard anatarijia mashabiki wa timu hiyo watazidi kuishangilia huku akifanya juhudi kuimarisha matokeo katika kipindi cha miezi miwili iliyobaki msimu kukamilika.
"Sitaki lionekane kama jambo la kawaida ila uhusiano wangu na mashabiki wa Chelsea unafahamika,” alisema.
"Nimekuwa mchezaji hapa kwa miaka 13, nimekuwa kocha hapa. Nimekuwa na kumbukumbu nzuri na pia nimekuwa na wakati mgumu. Hilo ni jambo la kawaida katika soka. Mashabiki wa Chelsea wamekuwa na mimi tangu nilipojiunga na klabu hii miaka mingi iliyopita. Nawashukuru sana kwa hilo.
"Iwapo tutaungana pamoja na kusaidia timu hii, tutakuwa na wakati mzuri na kurudisha kumbukumbu na mafanikio ya awali ugani Stamford Bridge kwa kipindi kilichosalia cha msimu. Hilo ndilo jukumu langu.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi za UEFA.
Mechi - 4
Real Madrid - 1
Chelsea - 2
Sare - 1
Ratiba ya mechi za UEFA:
Aprili 11 Jumanne
9:00pm: Benfica v Inter Milan
9:00pm: Manchester City v Bayern Munich
Aprili 12 Jumatano
9:00pm: Real Madrid v Chelsea
9:00pm: AC Milan v Napoli
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.