Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 Italian Serie A
Matchday 29
SS Lazio v Juventus FC
Stadio Olimpico
Spezia, Italy
Saturday, 8 April 2023
Kick-off is at 22h45
SS Lazio watamenyana vikali na Juventus FC kwenye
mechi ya ligi kuu Italia ugani Stadio Olimpico Aprili 9.
Matokeo ya hivi karibuni
The Eagles ambao ni Lazio walipata ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya AC Monza Aprili 2 huku wakiendeleza msururu wa mechi walizocheza bila kushindwa kwenye ligi hadi sita.
Vile vile, Lazio hawajapoteza mechi ya ligi katika michezo miwili iliyopita wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi wa mechi mbili mfululizo ugani Stadio Olimpico.
Juventus waliibuka na ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Hellas Verona Aprili 1 ikiwa ni ushindi wa tatu mfululizo kwao katika ligi.
The Old Lady wameshinda mechi mbili kati ya mechi tatu za mwisho walizocheza ugenini huku wakipoteza mchezo wa tatu.
Athari ya matokeo ya mechi hii.
Lazio wanapambana kumaliza mbili bora msimu huu katika ligi kwani wapo katika nafasi ya pili kwenye jedwali alama 16 nyuma ya viongozi SSC Napoli.
Lazio chini ya Maurizio Sarri itajihakikishia nafasi ya pili iwapo watapata ushindi dhidi ya Juventus ambao wapo katika hali nzuri kwa sasa.
Juventus wanashikilia nafasi ya saba kwa sasa na ushindi dhidi ya Lazio utapiga jeki matumaini yao ya kumaliza sita bora.
Habari ya vikosi
Mlinzi wa kati Mario Gila wa Lazio huenda akakosa mechi dhidi ya Juventus kutokana na jeraha la mguu. Zaidi ya hilo, Lazio haina mchezaji anayetumikia marufuku au adhabu.
Kwa upande mwingine, Juventus itawakosa wachezaji Kaio Jorge, Paul Pogba na Leonardo Bonucci ambao wanauguza majeraha.
Wachezaji muhimu
Matumaini ya Lazio yapo kwa mchezaji Ciro Immobile ambaye ni mfungaji wao bora msimu huu akiwa na magoli 9. Mshambuliaji huyo ana uwezo mkubwa wa kusaidia timu yake kupata ushindi dhidi ya Juventus.
Dusan Vlahovic ndiye mfungaji bora kwa upande wa Juventus akiwa na magoli 8. Raia huyo wa Serbia ataongoza safu ya ushambuliaji ya Juventus kusaka ushindi dhidi ya Lazio.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Nukuu
"Mechi hii haikuwa rahisi kama ilivyo kwa mechi zote za baada ya mapumziko ya ligi. Tulifahamu itakuwa mechi ngumu kwa sababu Verona wana uwezo wa kuharibu mtiririko wa mechi,” alisema meneja wa Juventus Massimiliano Allegri baada ya mechi dhidi ya Verona.
"Walituzuia dakika za kwanza ya mechi lakini tulifanikiwa kudhibiti mbinu zao na kutengeneza nafasi. Tulikuwa na nafasi ya kuongeza magoli zaidi bila kuwapa nafasi na muda wa kutekeleza mbinu zao kwenye himaya yetu.
"Ni sehemu tunayohitaji kuimarisha. Mechi inayofuata itakuwa dhidi ya Inter Milan. Muhimu zaidi ni kuwa wachezaji wetu wachanga wana uwezo mkubwa. Mpango wa Next Gen ni muhimu kwa kuwa unatupa fursa ya kuweleta wachezaji hawa kwenye kikosi cha kwanza siku zinazokuja.”
Takwimu baina ya timu hizi.
Juventus walipata ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya Lazio kwenye mechi yao ya mwisho ya ligi Novemba 13 2022 Allianz Stadium.
The Old Lady wamecheza mechi sita za ligi dhidi ya Lazio bila kupoteza hata moja baada ya kuandikisha ushindi mara nne na kupata sare mbili.
Ratiba ya mechi za ligi ya Italia Aprili 7-8
Aprili 7 Ijumaa
6:00pm - US Salernitana v Inter Milan
8:00pm - US Lecce v SSC Napoli
10:00pm - AC Milan v Empoli FC
Aprili 8 Jumamosi
13:30pm - Udinese Calcio v AC Monza
3:30pm - ACF Fiorentina v Spezia Calcio
5:30pm - Atalanta BC v Bologna FC
5:30pm - UC Sampdoria v US Cremonese
7:30pm - Hellas Verona v US Sassuolo
7:30pm - Torino FC v AS Roma
9:45pm - SS Lazio v Juventus FC
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.