La Liga - FC Barcelona v Atletico Madrid 


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 Spanish La Liga

Matchday 30

FC Barcelona v Atletico Madrid 

Spotify Camp Nou 
Barcelona, Spain 
Sunday, 23 April 2023 
Kick-off is at 16h15  
 
FC Barcelona itakabiliana vikali na Atletico Madrid kwenye mechi ya ligi kuu Uhispania ugani Spotify Camp Nou Aprili 23.
 
Matokeo ya hivi karibuni
 
Barca ilipata sare ya 0-0 ugenini dhidi ya Getafe CF katika mechi iliyochezwa Aprili 16 na sasa hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi sita zilizopita.
 
Vile vile, Barcelona hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi 14 zilizopita wakiwa nyumbani huku wakishinda mechi 11 na kupata sare 3 ugani Spotify Camp Nou.
 
Kwa upande mwingine, Atletico walishinda 2-1 wakiwa nyumbani dhidi ya UD Almeria Aprili 16 na kuifanya mechi ya 13 katika ligi bila kushindwa.
 
The Mattress Makers, kama wanavyofahamika Atletico hawajapoteza mechi ya ligi katika michezo 6 ugenini huku wakiandikisha ushindi katika mechi 4 na kupata sare 2.  
 
Athari ya matokeo ya mechi hii.
 
Barcelona wanazidi kuongoza jedwali la ligi ya La Liga kwa alama 11.
 
Watakuwa na lengo na kupanua nafasi hiyo zaidi watakapokutana na Atletico wakiwa na matumaini kuwa Real Madrid waliopo nafasi ya pili watapoteza alama dhidi ya Celta Vigo Aprili 23.
 
Atletico wapo katika nafasi ya tatu, alama 13 nyuma ya Barcelona na ushindi dhidi yao utapunguza alama hizo hadi 10.
 
Habari ya vikosi.
 
Ousmane Dembélé, Pedri, Frenkie de Jong na Sergi Roberto wa Barcelona wanauguza mejeraha na watakosa mechi hiyo. Zaidi ya mejeruhi, Barcelona hawana mchezaji anayetumikia adhabu.
 
Atletico watakosa huduma za wachezaji Reinildo Mandava na Memphis Depay lakini hawana mchezaji anayetumikia adhabu au marufuku.
 
Wachezaji muhimu
 
Macho yote yatamwangazia mshambuliaji Robert Lewandowski baada ya Barcelona kukosa kufunga goli katika mechi mbili mfululizo. Mchezaji huyo ana uwezo mkubwa wa kufunga magoli hivyo Barcelona wanamtegemea sana kwenye mechi hiyo.
 
Atletico wanamtazamia Aintoine Griezmann ambaye ameonyesha kiwango kikubwa msimu huu kwa kutoa pasi 8 zilizosababisha goli.
Antoine Griezmann
Hakimiliki ya picha: Getty Images


Nukuu
 
“Uwanja haukuwa mzuri kwetu. Tulitarajia hilo kwa sababu tulifanyia mazoezi kwenye uwanja mkavu Jumamosi. Sio rahisi kuchezea katika mazingira kama haya,” Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez alisema baada ya mchezo dhidi ya Getafe.
 
"Ni vigumu mpira kuteleza kwenye uwanja kama huo. Sio kwetu tu, hata kwa Getafe. Inasaidia sana kuwa na uwanja wenye nyasi nzuri. Alama moja sio matokeo mabovu ukizingatia mazingira hayo.
 
“Tumezoe kucheza pasipo na jua au usiku. Itatubidi kuzoea mazingira mapya. Jumapili ijayo tutacheza tena. Sio kisingizio lakini tutalazimika kuzoea hali hii mpya.”
 
Takwimu baina ya timu hizi
 
Barcelona walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Atletico walipokutana mara ya mwisho kwenye mchezo wa ligi mnamo Januari 8 2023 ugani Cívitas Metropolitano.
 
Barca hawajapoteza dhidi ya Atletico katika michezo miwili ya ligi iliyopita huku wakiandikisha ushindi mara mbili mfululizo.
 

Ratiba ya mechi za La liga mchezo wa 30.


Aprili 21 Ijumaa

10:00pm- RCD Espanyol v Cadiz CF

Aprili 22 Jumamosi

3:00pm - CA Osasuna v Real Betis
5:15pm- UD Almeria v Athletic Bilbao
7:30pm- Real Sociedad v Rayo Vallecano
7:30pm- Real Valladolid v Girona FC
10:00pm- Real Madrid v Celta Vigo

Aprili 23 Jumapili

3:00pm - Elche CF v Valencia CF
5:15pm - FC Barcelona v Atletico Madrid
7:30pm - Real Mallorca v Getafe CF
10:00pm - Sevilla FC v Villarreal CF 
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 04/21/2023