F1 - 2023 Azerbaijan Grand Prix


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2023 FIA Formula One World Championship

2023 Azerbaijan Grand Prix

Baku City Circuit
Baku, Azerbaijan
Sunday, 30 April 2023
 
Dereva wa Red Bull Racing, Max Verstappen anapania kumaliza katika nafasi ya jukwaani kwa mara ya nne mfululizo huku akifukuzia ushindi wa pili mfululizo kwenye mbio za langa langa za Azerbaijan Grand Prix Jumapili Aprili 30.
 
Verstappen ambaye ni bingwa mara mbili wa dunia wa Formula One alishinda mbio za langa langa za mkondo wa Baku City Circuit msimu uliopita. Hii ni baada ya kushiriki mbio nne za awali bila mafanikio yoyote.
 
Verstappen anaongoza kwenye jedwali la dunia la madereva, alama 15 mbele ya dereva mwenza wa Red Bull Sergio Perez baada ya kushinda mbio za Bahrain Grand Prix pamoja na Australian Grand Prix huku akichukua nafasi ya pili ya katika mbio za Saudi Arabian Grand Prix.

Sergio PerezHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Fernando Alonso wa Aston Martin ameonyesha ushindani mkubwa akiwakilisha timu yake mpya baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio tatu mfululizo na sasa yupo katika nafasi ikiwa ni alama tisa nyuma ya Perez.
 
Mbio za tatu za msimu zilijawa na visanga vilivyopelekea huduma za gari la kuhakikisha usalama kuhitajika baada ya migongano na ajali kutokea mara kadhaa japokuwa Verstappen alijitahidi sana na kumaliza mbele ya Lewis Hamilton kwa sekunde chache sana.
 
Raia huyo wa Uholanzi alianza mbio akiwa katika nafasi ya kwanza ila akapoteza nafasi hiyo kwa George Russell na Hamilton wote wa Mercedes baada ya muda mfupi ambao alilalamika kuwa walivunja kanuni kwa kufanya hivyo katika mzunguko wa kwanza.
 
"Binafsi nilijaribu kuepuka kugongana. Kanuni zipo wazi kinachohitajika unapotaka kumpita mwenzako upande wa nje lakini hazitiliwi maanani,” alisema Verstappen said.
 
"Sina tatizo. Tulikuwa na kasi nzuri na baadaye tulifanikiwa kumpita Hamilton ila hayo yanafaa kuzingatiwa katika mbio zijazo.”
 

Matokeo yam bio za Australian Grand Prix 2023:

 
Mshindi: Max Verstappen - Red Bull Racing
Nafasi ya pili: Lewis Hamilton - Mercedes
Nafasi ya tatu: Fernando Alonso - Aston Martin
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 04/26/2023