Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 32
Newcastle United v Tottenham Hotspur
St James' Park
Newcastle upon Tyne, England
Sunday, 23 April 2023
Kick-off is at 15h00
Newcastle watakuwa wenyeji wa Tottenham katika
mechi ya Premier ugani St James' Park Jumapili Aprili 23 huku timu zote mbili zikiwania nafasi ya kushiriki ligi ya UEFA msimu ujao.
Awali, the Magpies walikuwa wameshinda mechi tano za ligi mfululizo na kuwapiku Manchester United katika nafasi ya tatu kwenye jedwali.
Hata hivyo, Newcastle chini ya Eddie Howe iliteleza kidogo baada ya kupokea kichapo cha 3-0 mikononi mwa Aston Villa, Villa Park Jumamosi iliyopita na sasa wapo nafasi ya nne, alama tatu nyuma ya Red Devils waliopata ushindi wa 2-0 dhidi ya Nottingham Forest siku iliyofuata.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Spurs wapo katika nafasi ya 5, alama 3 nyuma ya Newcastle walio na mchezo mmoja mkononi. Hii ni baada ya Spurs kupoteza 3-2 dhidi ya Bournemouth wikendi iliyopita
Aston Villa wanachukua nafasi ya 6 baada ya kushinda mechi tano mfululizo na sasa wapo mbioni kushiriki mashindano ya ligi za ulaya.
Kabla ya mechi dhidi ya Bournemouth, Tottenham chini ya ukufunzi wa Cristian Stellini ilikuwa imeshiriki mechi nne za ligi bila kupoteza hata moja na mechi dhidi ya Newcastle itawapa fursa kujikwamua.
Alexander Isak alionyesha mwanzo mzuri na timu ya Newcastle kwani alifanikiwa kufunga magoli mawili katika mechi tatu za kwanza kabla ya jeraha la paja kumuweka nje ya uwanja kwa miezi mitatu. Raia huyo wa Sweden amefunga magoli sita katika mechi 11 tangu kurejea mwezi Januari na kumuweka nje ya kikosi Cullum Wilson.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Son Heung-Min hajaonyesha ubora uliompelekea kushinda kiatu cha dhahabu kwa pamoja msimu uliopita alipofunga magoli 23. Mshambuliaji huyo wa Korea kusini amefunga magoli 8 tu katika mechi 29 msimu huu. Son amefunga goli moja dhidi ya Brighton na pia Bournemouth katika mechi mbili zilizopita.
Katika vikosi, Newcastle watamkosa Allan Saint-Maximin (paja) na pia Emil Krafth (goti) kwenye pia hiyo huku Tottenham wakikosa huduma za wachezaji Emerson Royal, Rodrigo Bentancur (goti), Ryan Sessegnon, Ben Davies (paja), Yves Bissouma (kisigino) na Clement Lenglet ambaye ana jeraha la misuli. Lucas Moura anatumikia adhabu hivyo basi atakosa mechi hiyo vile vile.
Kocha wa Newcastle Howe anataka kuona timu yake ikijizoa baada ya matokeo mabovu dhidi ya Aston Villa huku akikiri kuwa ulikuwa mchezo wa kutamausha sana ukilinganisha na michezo mengine msimu huu.
"Ndio, nahisi kilikuwa kiwango cha chini kabisa tulichoonyesha msimu huu. Hatukucheza vizuri katika mechi muhimu,” alisema. “Wachezaji hawa wamekuwa wakionyesha mchezo mzuri mara nyingi msimu huu. Hali kama hii inaweza kutokea. Tunahitaji kujituma zaidi na kusahihisha makosa yetu kwenye mechi ijayo.
"Tuliadhibiwa kwa utepetevu wetu na timu nzuri. Hatukucheza kwa viwango ambavyo tumekuwa tukionyesha siku zote. Tulipoteza mpira ovyo na kufanya maamuzi yaliyotugharimu. Hatukuzuia na kudhibiti wapinzani wetu kikamilifu.
"Haikuwa siku yetu leo. Tutachambua mchezo huu na kutafuta suluhisho. Katika kipindi hiki cha msimu ambapo mechi chache sana zimesalia, muhimu ni kuzingatia yanayokuja na kusahau yaliyopita.”
Mkufunzi wa Tottenham Stellini alihisi kuwa timu yake ilistahili ushindi dhidi ya Bournemouth baada ya kujituma na kujitolea huku lawama kwa timu yake ikiwa hawakufunga zaidi ya mawili.
"Tulipambana sana. Wachezaji wangu hawana cha kujutia baada ya kuonyesha mchezo kama wa leo. Wanachotakiwa kufanya ni kucheza vizuri tangu mwanzo hadi mwisho wa mechi bila kuyumba,” raia huyo wa Italia aliambia SPURSPLAY.
"Baada ya kufunga goli la pili tulilegea sana na kuwaruhusu kufunga magoli mawili. Sio rahisi kujikomboa kutoka hali hiyo. Tulijituma kwa nguvu kubwa baadaye na tulikuwa na nafasi ya kushinda kupitia mchezaji Richarlison vile vile.
"Tulitengeneza nafasi nyingi za kutupatia ushindi na tulistahili kushinda mechi hiyo. Usipotengeneza nafasi hizo basi unakuwa na hujacheza vizuri. Tulitengeneza nafasi na kufunga goli la pili na pia Richarlison alipata nafasi nzuri dakika za mwisho."
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Newcastle - 1
Tottenham - 2
Sare - 2
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 32:
Aprili 21 Ijumaa
10:00pm: Arsenal v Southampton
Aprili 22 Jumamosi
2:30pm: Fulham v Leeds United
5:00pm: Brentford v Aston Villa
5:00pm: Crystal Palace v Everton
5:00pm: Leicester City v Wolverhampton Wanderers
5:00pm: Liverpool v Nottingham Forest
Aprili 23 Jumapili
4:00pm: Bournemouth v West Ham United
4:00pm: Newcastle United v Tottenham Hotspur
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.