Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 31
West Ham United v Arsenal
London Stadium
London, England
Sunday, 16 April 2023
Kick-off is at 16h00
Viongozi wa
ligi ya Premier Arsenal watakuwa na kibarua kigumu watakapoikabili West Ham London Stadium katika mechi ya ligi mnamo Aprili 16, Jumapili.
Nafasi kati ya the Gunners na Manchester City ambao wanashika nafasi ya pili ilipungua hadi alama sita baada ya viongozi wa ligi kutoa sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool Jumapili iliyopita ugani Anfield.
Kuna uwezekano alama hizo zitapungua hadi tatu iwapo City watashinda mechi yao ya mkononi, ikiwa wameshinda mechi tano za ligi mfululizo baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Southampton Jumamosi iliyopita.
Kabla ya mechi dhidi ya Liverpool, Arsenal chini ya Mikel Arteta walikuwa wameshinda mechi saba mfululizo na kupiga jeki azma ya kushinda taji la ligi kwa mara ya kwanza tangu msimu 2003-04.
Newcastle waliopo katika nafasi ya 3 na Manchester United nafasi ya 4 walipata ushindi kwenye mechi zao dhidi ya Brentford na Everton mtawalia.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
The Hammers walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Fulham ugani Craven Cottage na kuongeza nafasi ya kusalia katika ligi baada ya kupata kichapo kikubwa cha 5-1 mikononi mwa Newcastle hapo awali.
Ushindi wa tatu ndani ya mechi sita umeipeleka timu hiyo chini ya David Moyes hadi nafasi ya 14, alama tano juu ya mstari wa kushushwa daraja huku wakiwa juu ya Bournemouth kwa ubora wa magoli wote wakiwa na alama 30.
Wolves wapo katika nafasi ya 13, Crystal Palace nafasi ya 12 huku Chelsea wakishika nafasi ya 11.
Mshambuliaji wa zamani wa City Gabriel Jesus anazidi kuwa na mchango mkubwa kwa timu ya Arsenal baada ya kufunga magoli 8 na kuchangia kupatikana magoli 6 katika michezo 18 ya ligi tangu alipohamia timu hiyo. Raia huyo wa Brazil amefunga dhidi ya Liverpool katika mechi mbili mfululizo na sasa amefunga mabao matatu tangu kurejea uwanjani baada ya jeraha la goti mwezi jana.
West Ham wamekuwa katika hali ngumu ya upatikanaji wa magoli. Ni miongoni mwa timu zilizo na uhaba wa magoli. Said Benrahma ni mfungaji bora kwa pamoja na Jarrod Bowen wakiwa na magoli 4. Mkwaju wa penalti uliosawazisha dhidi ya Aston Villa Machi 12 lilikuwa goli la kwanza la raia huyo wa Algeria katika mechi tisa.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwenye vikosi, West Ham watamkosa mchezaji Gianluca Scamacca anayeuguza jeraha la goti. Haijabainika wazi iwapo Lucas Paqueta atakuwa amepona kushiriki mechi hiyo. Takehiro Tomiyasu, Mohamed Elneny wanauguza jeraha la goti, Eddie Nketiah anauguza jeraha la kisigino pamoja na William Saliba watakosa mechi hiyo kwa upande wa timu ya Arsenal.
The Hammers walizuia vizuri dhidi ya Fulham kwa dakika 60 na kupata ushindi wa pili wa msimu huu ugenini. Moyes alisifia safu yake ya ulinzi kwa juhudi walizoonyesha japokuwa alisema wanahitaji kuimarisha uchezaji wao.
"Unaposhambuliwa unahitaji kutafuta suluhu. Unahitaji walinzi wanaofahamu jinsi ya kutatua changamoto. Wanaofahamu majukumu yao na wanachohitajika kufanya. Wachezaji wangu walielewa jukumu lao vizuri leo,” alisema raia huyo wa Scotland.
"Ukiangalia takwimu ni dhahiri kwamba vijana walijituma vilivyo ila tunahitaji kucheza vizuri zaidi.”
Arteta alikiri kuwa walibahatika sana kupata alama moja dhidi ya Liverpool baada ya Mohamed Salah kukosa tuta la penalti kipindi cha pili.
"Unaporuhusu goli katika dakika za mwisho ni wazi kuwa alama mbili zimepotea. Unajutia nafasi ambazo hukutumia vizuri,” alisema raia huyo wa Uhispania.
"Liverpool walipata nafasi nne za wazi kabisa ila hawakufunga. Walikosa penalti pia. Tulikuwa na nafasi ya kucheza na kufanya vizuri kipindi cha pili. Hatukufanya hivyo.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi - 5
West Ham - 0
Arsenal - 4
Sare - 1
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 31:
Aprili 15 Jumamosi
1:30pm: Aston Villa v Newcastle United
4:00pm: Chelsea v Brighton & Hove Albion
4:00pm: Everton v Fulham
4:00pm: Southampton v Crystal Palace
4:00pm: Tottenham Hotspur v Bournemouth
4:00pm: Wolverhampton Wanderers v Brentford
6:30pm: Manchester City v Leicester City
Aprili 16 Jumapili
3:00pm: West Ham United v Arsenal
5:30pm: Nottingham Forest v Manchester United
Aprili 17 Jumatatu
9:00pm: Leeds United v Liverpool
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.