EPL - Manchester City v Arsenal


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 33

Manchester City v Arsenal

Etihad Stadium
Manchester, England
Wednesday, 26 April 2023
Kick-off is at 21h00 
 
Manchester City watakuwa mwenyeji wa Arsenal ugani Etihad Stadium katika mechi za ligi mnamo Jumatano Aprili 26.
 
The Gunners walitoka sare ya 3-3 na Southampton kwenye mechi ya ligi Ijumaa iliyopita ugani Emirates na sasa wanatenganishwa na alama 5 tu baina yao na City kutoka alama 11.
 
Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu katika michezo mitatu ya ligi kwa vijana wa Arteta kupata sare huku awali wakitoa sare dhidi za Liverpool na West Ham na kuwapa City nafasi murua ya kutetea taji la ligi.


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
Suggested photo: Riyad Mahrez of Manchester City
 
City ambao ni mabingwa watetezi wana michezo miwili mkononi na iwapo watashinda mechi ya marudiano dhidi ya Arsenal, nafasi kati yao itapungua hadi alama mbili. Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizi, City waliibuka na ushindi wa 3-1 mnamo Februari 15.
 
City chini ya Pep Guardiola walifuzu kucheza katika fainali ya kombe la FA kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Sheffield United Jumamosi iliyopita na sasa watarudi kwenye kibarua cha kusaka taji la saba la ligi katikati mwa juma.
 
Riyad Mahrez alifunga magoli yote matatu dhidi za Sheffiled kwenye mechi ya nusu fainali ya FA na anatarajia kuendelea kubaki kikosini kwani amelazimika kuwa mchezaji wa akiba miezi ya hivi karibuni kutokana na uchezaji mzuri wa Phil Foden.

Gabriel Martinelli
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Gabriel Martinelli amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Arsenal msimu huu na amefanikiwa kucheza mechi zote za ligi isipokuwa mechi tatu tu katika mechi 32 msimu huu. Raia huyo wa Brazil alifunga goli lake la 15 la ligi msimu huu na la nane katika mechi 10 walipotoka sare ya 3-3 dhidi ya Saints.
 
Katika habari ya vikosi, Nathan Ake anauguza jeraha la paja na atakuwa mchezaji wa pekee kukosa mechi hiyo kwa upande wa City. Arsenal watakosa huduma za Takehiro Tomiyasu na Mohamed Elneny kwa majeraha ya goti. William Saliba anauguza maumivu ya mgongo. Haijabainika wazi kama kiungo mkabaji Granit Xhaka atashiriki mechi hiyo kutokana na ugonjwa.
 
Guardiola anatumai wachezaji wake wote watakuwa wazima wa afya kuchangia kadri wawezavyo katika azma ya kutetea taji lao la ligi baada ya Foden kurejea uwanjani kipindi cha pili dhidi ya Sheffield. Foden alikuwa nje kwa muda baada ya kufanyiwa upasuaji.
 
"Lengo letu ni kushiriki mchezo baada ya mchezo na kila mchezaji kuweza kuchangia. Hatuna majeruhi kwa sasa," alisema raia huyo wa Uhispania. "Phil Foden amepona. Tunaweza kuwategemea wachezaji Sergio Gomez na Stefan Ortega Moreno vile vile. Kila mmoja atakuwa na mchango wake."
 
Arteta anasisitiza kuwa wachezaji wake wana uchu wa kushinda taji na wataongeza juhudi mara dufu watakapocheza na City Jumatano.
 
"Wanataka ubingwa sana. Sio wachezaji tu, bali pia mashabiki na wafanyakazi wetu. Nafahamu kuwa sio rahisi," alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Kila mmoja atapumzika leo na kesho tutaanza maandalizi na mbinu za kupata ushindi dhidi ya Manchester."
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Man City - 5
Arsenal - 0
Sare - 0
 

Ratiba ya mechi za mchezo wa 33:

 
Aprili 25 Jumanne
 
8:30pm: Wolverhampton Wanderers v Crystal Palace
 
8:45pm: Aston Villa v Fulham
 
9:00pm: Leeds United v Leicester City
 
Aprili 26 Jumatano
 
8:30pm: Nottingham Forest v Brighton & Hove Albion
 
8:45pm: West Ham United v Liverpool
 
8:45pm: Chelsea v Brentford
 
9:00pm: Manchester City v Arsenal
 
Aprili 27 Alhamisi
 
8:45pm: Everton v Newcastle United
 
8:45pm: Southampton v Bournemouth
 
9:15pm: Tottenham Hotspur v Manchester United
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 04/26/2023