Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 30
Liverpool v Arsenal
Anfield
Liverpool, England
Sunday, 9 April 2023
Kick-off is at 18h30
Arsenal wanatarajia kupiga jeki azma ya kushinda
taji la Premier tangu msimu 2003-04 watakapocheza na Liverpool ugani Anfield Jumapili Aprili 9.
The Gunners wamekuwa na msimu mzuri hadi kufikia sasa huku wakishinda mechi 23 kati ya mechi 29 na sasa wanaongoza jedwali alama nane mbele ya bingwa mtetezi Manchester City.
Hadi sasa, Mikel Arteta amepoteza mechi tatu tu za ligi huku ushindi wa 4-1 dhidi ya Leeds ugani Emirates Jumamosi iliyopita ukifikisha msururu wa mechi saba bila kushindwa kwa Arsenal tangu walipopoteza 3-1 dhidi ya Manchester City Februari 15.
Shindano hili linadhihirisha kuwa baina ya timu mbili baada ya Manchester United kupoteza 2-0 dhidi ya Newcastle United Jumapili iliyopita.
The Magpies wanachukua nafasi ya tatu, mbele ya United kwa ubora wa magoli huku timu zote mbili zikiwa na alama 50, alama 14 nyuma ya Citizens na alama 22 nyuma ya viongozi wa ligi Arsenal.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Juhudi za The Reds kumaliza nne bora kwenye ligi zilitumbukia nyongo baada ya kupoteza 4-1 dhidi ya City wikendi iliyopita. Kabla ya mechi dhidi ya City, Liverpool walipoteza 1-0 mikononi mwa Bournemouth hapo awali.
Kati ya Februari 18 na Mach 5i, Vijana wa Jurgen Klopp walicheza mechi tano za ligi bila kupoteza na kujipa matumaini zaidi ila matokeo ya hivi punde yamewaacha nafasi ya nane kwenye jedwali, alama nane chini ya nafasi ya kushiriki ligi ya klabu bingwa ulaya.
Brighton (6) na Brentford (7) wapo alama moja mbele ya Liverpool walio na alama 42. Aston Villa wapo nafasi ya 9 na alama 41, Fulham nafasi ya 10 na alama 39 huku Chelsea wakishika nafasi ya 11 na alama 38.
Mohamed Salah aliandikisha rekodi nyingine na Liverpool baada ya kumpiku Michael Owen na kuwa mchezaji mwenye magoli mengi ya ligi ya ugenini alipofunga dhidi ya Manchester City wikendi iliyopita. Raia huyo wa Misri anaonekana kurudia makali yake baada ya kuanza msimu vibaya na sasa amefunga magoli 12 kwenye mechi 27.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Baada ya kuwa nje kwa miezi 4 kutokana na jeraha la goti, Gabriel Jesus alirejea uwanjani na kufunga mawili dhidi ya Leeds na kufikisha idadi ya magoli saba msimu huu pamoja na kusaidia kupatikana magoli sita kwa ujumla.
Kwenye habari ya vikosi, Naby Keita alipata jeraha akichezea taifa lake la Guinea na anajumuika na wachezaji Calvin Ramsay, Luis Diaz (wote jeraha la goti), Stefan Bajcetic na Thiago Alcantara (jeraha la kinena) kwenye meza ya matibabu hivyo watakosa mechi hii kwa upande wa Liverpool. Arsenal watakosa huduma za Takehiro Tomiyasu, Mohamed Elneny (goti), Eddie Nketiah (kisigino) na William Saliba anayeuguza jeraha la mgongo.
Klopp anawataka wachezaji wake kuwa na umakini zaidi kwani wamekuwa wakiruhusu magoli ya mapema kwenye mechi nyingi msimu huu na kufanya mchezo kuwa mgumu.
"Tunatakiwa kucheza vizuri wakati wote na sio baadhi ya mechi tu. Ulegevu wa aina yoyote kwenye ligi ya Premier unaadhibiwa na timu pinzani,” alisema raia huyo wa Ujerumani.
"Ni hali tunayojikuta wakati huu ambayo tulizungumzia jana (Ijumaa). Ni hali ambayo sitaki kuizungumzia lakini pia siwezi kuipuuza.”
Katika mbio za ubingwa, Arteta alidokeza anachukua hali hii mechi baada ya mechi ili kuhakikisha wachezaji wake wapo katika hali nzuri kiakili kwenye kila mechi.
"Tunafurahia tulipo kwa sasa,” alisema raia huyo wa Uhispania. “Imesalia michezo 9 ila Jumatatu tutakuwa na siku ya mazoezi ambayo itatuwezesha kuimarika kama kikosi. Mechi baada ya mechi wachezaji wanakuwa katika hali nzuri kiakili kwa ajili na kibarua kijacho.
"Unahema vizuri na sio kung’ang’ana kuvuta pumzi. Tunahitaji kuwa na imani na nguvu ya kufanikisha hilo kadri mechi zinavyokuja.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Liverpool - 4
Arsenal - 1
Sare - 0
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 30:
Aprili 8 Jumamosi
2:30pm: Manchester United v Everton
5:00pm: Aston Villa v Nottingham Forest
5:00pm: Brentford v Newcastle United
5:00pm: Fulham v West Ham United
5:00pm: Leicester City v Bournemouth
5:00pm: Tottenham Hotspur v Brighton & Hove Albion
5:00pm: Wolverhampton Wanderers v Chelsea
7:30pm: Southampton v Manchester City
Aprili 9 Jumapili
4:00pm: Leeds United v Crystal Palace
6:30pm: Liverpool v Arsenal
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.