Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 Zurich Classic of New Orleans
US PGA Tour
TPC Louisiana
Avondale, Louisiana, USA
22 - 25 April 2022
Shindano la gofu la mwaka
2022 la Zurich Classic of New Orleans linatarajiwa kuchezewa TPC Louisiana iliyopo Avondale katika jimbo la Louisiana Marekani kati ya tarehe 22 na 25 Aprili.
Shindano hili liliasisiwa mwaka 1938 na limekuwa likiandaliwa kila mwaka tangu mwaka 1958 lakini shindano la mwaka 2022 halikufanyika kutokana na janga la Corona. Mfadhili kuu wa shindano hili ni Zurich Insurance Group.
Shindano la gofu la Zurich Classic limekuwa shindano la makundi tangu mwaka 2017, likiwa na timu themanini za wachezaji wawili. Zawadi ya shindano la mwaka huu ni dola milioni 8 huku mshindi akipokea dola 1,199,350 kila mmoja.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
March Leishman na Cameron Smith ndio mabingwa watetezi wa Zurich Classic of New Orleans baada ya kushinda shindano la mwaka 2021 kwa kuwashinda wachezaji wa Afrika Kusini Louis Oosthuizen na Charl Schwartzel katika hawamu ya muondoano.
Viktor Hovland, Collin Morikawa, Cameron Smith, Scottie Scheffler, Patrick Cantlay watashiriki shindano la mwaka huu ambalo litakuwa ni shindano la pekee litakalo husisha vikundi kwenye ratiba ya PGA Tour msimu wa 2021-22.
Shindano litahusisha wachezaji 160 na litachezwa kwa siku nne. Timu themanini za wachezaji wawili zitakuwa uwanjani, vikundi vinne na mipira minne wakipishana kwa siku, kwa mizunguko minne itakayojumuisha matundu 36 ili kuamua mshindi.
Baadhi ya makundi hayo ni pamoja na Collin Morikawa na Hovland, Max Homa na Talor Gooch, Jason Day na Jason Scrivener, Smith na Leishman, Sergio Garcia na Tommy Fleetwood, Scheffler na Ryan Palmer bila kuwasahau Joaquin Niemann na Mito Pereira.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Justin Rose ambaye alishinda shindano la mchezaji mmoja la Zurich Classic mwaka 2015 ataungana tena na Henrik Stenson kwa mara ya nne katika shindano hili.
“Wachezaji hawa wawili wameshinda mataji makubwa katika maisha yao ya uchezaji na walikuwa wa kwanza kujitolea kama timu shindano lilipobadili mfumo mwaka 2017,” alisema Steve Worthy, ambaye ni mkurugenzi wa shindano la Zurich Classic.
“Wameshirikiana kupata mafanikio makubwa katika Ryder Cup, na sasa Henrik atakuwa nahodha wa timu ya Ulaya katika shindano la mwaka 2023.”
Hakuna mchezaji aliyefanikiwa kushinda shindano hili mara tatu lakini wachezaji kumi wameshinda mara mbili. Wachezaji hao ni; Henry Picard, Byron Nelson, Bo Wininger, Frank Beard, Billy Casper, Tom Watson, Chip Beck Ben Crenshaw, Carlos Franco na Billy Horschel.
Washindi 5 wa mwisho wa Zurich Classic of New Orleans
2016 - Brian Stuard - Marekani
2017 - Cameron Smith - Australia na Jonas Blixt - Uswidi
2018 - Billy Horschel na Scott Piercy - Marekani
2019 - Ryan Palmer - Marekani na Jon Rahm - Uhispania
2021 - Cameroon Smith na Marc Leishman - Australia
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.