Hakimiliki ya picha: Getty Images
WBC and The Ring heavyweight titles
Tyson Fury v Dillian Whyte
Professional Boxing Match
Wembley Stadium
London, England
Saturday, 23 April 2022
Bingwa wa muda wa mkanda wa WBC katika mchezo wa ndondi Dillian Whyte atakabiliana na Tyson Fury Aprili 23 ugani Wembley. Watakuwa wakishindania mkanda wa
WBC na mikanda mingine ya uzani wa heavyweight.
The Bodysnatcher, kama anavyofahamika Dillian Whyte amekuwa bingwa wa muda wa mkanda wa WBC tangu alipomshinda Alexander Povetkin mwezi Machi mwaka 2021, ambao ulikuwa ni ushindi wa kulipa kisasi kwani Alexander Povetkin alikuwa amemshinda Whyte katika pambano la kwanza Agosti 2020.
Whyte alishinda mkanda wa WBC wa muda kwa mara ya kwanza Julai 2019, heavyweight alipomshinda Oscar Rivas kabla ya kupoteza kwa Povetkin miezi 13 baadaye.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mwanamasumbwi huyo mwenye miaka 34 ambaye ni bingwa wa zamani wa kickboxing ameshinda mapambano 28 kati ya 30 aliyoshiriki huku akipoteza kwa Anthony Joshua Disemba 2015 na Povetkin Agosti 2020.
Whyte alikosa kuhudhuria kikao cha kwanza na wanahabari Machi 1 na kusema kuwa Fury hawezi kufanikiwa kumchezea michezo ya kisaikolojia wiki hii.
"Hawezi kufanikiwa kunichezea michezo ya kisaikolojia kwa sababu kiakili niko imara kabisa,” alisema Whyte ambaye ni muingereza mwenye asili ya Jamaica.
Hata baada ya kukiri kuwa Fury ni mwanamasumbwi bora wa kizazi hiki, Whyte amesema kuwa watu wamepitiliza kwa sifa wanazompa Fury kwani yeye anamuona kawaida tu.
"Ni mwanamasumbi mzuri. Ni yeye peke yake aliyeshinda mataji yote katika kizazi hizi. Ni mkubwa wa umbo na hajawai kushindwa,” alisema mchezaji huyo wa zamani wa mixed martial artist.
"Siamini katika sifa zote anazopewa. Yeye sio Muhammad Ali, Mike Tyson au Joe Frazier kama wengi wanavyomchukulia. Siamini kabisa.”
Rekodi yao katika masumbwi
Fury: 31–0–1 (22 KOs)
Whyte: 28–2 (19 KOs)
Bashiri ndondi na Betway
Tunakuletea mapambano bora ya ndondi na unaweza kubashiri kwa kutumia simu au kompyuta yako. Weka ubashiri wako kwa urahisi na uwashangilie mabondia unaowapenda kiganjani mwako. Betway inakupa kile unachotaka kwenye Ulimwengu wa kubashiri ndondi live. Rusha ngumi na ingia ulingoni nasi tunakupa odds nono. Bashiri kwenye mapambano makubwa na Betway Tanzania.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway